24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nape kumwakilisha Rais Samia Tamasha la Pasaka

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Rais Dk. Samia Suluhu Hssan katika Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Jumapili ya Aprili 9, mwaka huu Viwanja vya Leaders Clab Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.

Mkurugenzi wa Msama Promotion inayoratibu tamasha hilo, Alex Msama amewaambia Wwaandishi wa Habari mapema leo Aprili mosi, jijini Dar es Salaam kuwa, awali mgeni rasmi alipaswa kuwa Rais Samia lakini kutokana na majukumu atawakilishwa na Waziri Nape.

“Tamasha la Pasaka linatarajiwa kuhfanyika Jumapili ya Aprili 9, na mgeni rasmi atakuwa ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye atamuwakilisha Mhe. Rais mama yetu Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Niseme tu kwamba maandalizi ya tamasha hili yamekamilika kwa asilimia 100 na sasa kilichobaki ni watu kujiandaa na tamasha hili, wajitokeze kwa wingi kwani itakuwa ni bure kabisa hakuna kiingilio,” amesema Msama.

Katika hatua nyingine Msama amesema waimbaji wote wapo tayari na wameshaanza kuwasili nchini na mazoezi yanaendelea kwa ajili ya kukonga nyoyo za Watanzania kwenye tamsha hilo huku akidokeza kuwa kutakuwa na michezo.

“Msisahau kuwa kutakuwa na michezo ya kutosha kwa watoto, hivyo wazazi msiwaache watoto nyumbani kwani mtakuwa mnaburudika huku wao wakiwa wanacheza, pia kuna vyakula vya kutosha vitapatikana kwa bei nafuu,” amesema Msama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles