25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ujue ugonjwa wa Sikoseli na tiba yake

sickle-cell

Na Dk.  Deogratias Soka,

UGONJWA wa selimundu(sikoseli)  ni ugonjwa   wa kurithi ambao chimbuko lake ni  familia kuwa na mtu anayekuwa na ugonjwa husika.

Ugonjwa huo unaambatana na dalili nyingi zinazotokana na kuvunjika kwa seli na kukwama kwenye mishipa ya damu kutokana na umbile lake.

Mgonjwa asipopata matibabu ya haraka na uangalizi wa karibu wa wahudumu wa afya na walezi wa wagonjwa hawa dalili hizi huchangia kwa kiasi kikubwa kwa waathirika wa ugonjwa huu kulazwa hospitali mara kwa mara na vifo vya utotoni.

Athari za ugonjwa wa sikoseli

Maumivu

Chembe nyekundu za selimundu hushindwa kupitika kwa urahisi katika mishipa midogo ya damu na hivyo kukwama na kuziba mzunguko wa damu. Hali hii husababisha maumivu yenye ukali tofauti.

Maambukizi ya vimelea vya magonjwa:

Wagonjwa wa sikoseli hasa watoto hupata maambukizi ya vimelea vya magonjwa  mbalimbali  kama vichomi (pneumonia), homa ya uti wa mgongo na homa ya ini.

Upungufu wa damu

Kutokana na chembe nyekundu za  sikoseli kuwa na muda mfupi wa kuishi hii humuweka mgonjwa wa sikoseli katika hatari ya  kupata upungufu mkubwa wa  damu.

Kuvimba kwa mikono na miguu:

Mara nyingi huambatana na homa hali hii husababishwa na chembe nyekundu za sikoseli kukwama na kuziba mzunguko wa damu kwenda kwenye mikono na miguu.

Itaendelea wiki ijayo…

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles