24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mfundishe mtoto kufanya kazi ndogondogo

time-together

NA AZIZA MASOUD,

MZAZI ama mlezi ana nafasi kubwa ya kumjengea mtoto msingi  kwa kumfundisha vitu mbalimbali  ambavyo vitamjengea msingi mzuri.

Kuna vitu ambavyo watoto huelekezwa kwakuambiwa  kwa maneno na vingine anapaswa kumuelekeza kwa vitendo ili aweze kujifunza.

Vitu vya muhimu ambavyo mtoto anapaswa kufundishwa ni pamoja na kufanya kazi ndogondogo ambazo zinaweza kumjengea njia ya kujitengenezea mazingira ya kujituma anapokuwa mkubwa.

Baadhi ya wazazi hufanya makosa  kuajiri watu wa kufanya shughuli hizo wakati wanajua wana watoto wanaohitaji mafunzo katika kipindi ambacho anaanza kukua.

Mzazi anapaswa  kumfundisha mtoto  kufanya kazi ndogondogo ambazo zitamjenga na kumchangamsha akili kuanzia umri wa miaka mitano na kuendele.

Kila siku zinazoenda mtoto anapaswa kujifunza  vitu vipya kwakuwa kuna  umri ambao utafikia anapaswa  awe anajua ama kuwa na mwanga wa kujitegemea mwenyewe kufanya vitu mbalimbali hasa kazi za nyumbani.

Kuna kazi ndogo ndogo ambazo unaweza kumfundisha  kama kuosha vyombo  unaweza kuanza kumfundisha   kuosha kikombe chake baada ya kunywa  chai na sahani ya aliyotumia baada ya kula.

Kazi nyingine ambazo mtoto anaweza kufundishwa kufanya usafi wa  wa mazingira  kama kufyeka majani, kupalilia maua na bustani, kufagia nk.

Pia mtoto anaweza kufundishwa kufua kwakuanza nguo ndogo ndogo kama chupi,tisheti zake za ndani  na nyinginezo.

Mbali na hilo pia unaweza kumuelekeza  kupiga deki katika maeneo ya kawaida mfano chumbani kwake,kufuta meza hivyo vyote sio adhabu bali ni njia  mojawapo ya kumfundisha kazi.

Kwa upande wa kupika mtoto anapofika darasa la tano anapaswa aanze kujifunza  kujipikia  chakula chake mwenyewe anapotoka shule  mfano ugali  ama wali ambao utakuwa hauzidi mtu mmoja .

Wazazi wanapaswa kujua shughuli  ndogo ndogo za nyumbani huwajenga vijana kiakili,kiafya pia itamfanya mtoto awe na ujasiri unapompeleka kuishi mazingira tofuati na nyumbani.

Kuna haja ya wazazi kuamka katika hili kwani kuna familia ambazo mtoto mpaka anamaliza kidato cha nne hawezi kupika ugali hata wa kula mtu mmoja jambo ambalo ni aibu sana katika ulimwengu wa sasa.

Kumfundisha mtoto kazi sio kumchukia bali ni kumjengea msingi imara ambao utakuja kumsaidia katika maisha yake ya baadae.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles