28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

UGANDA KUFUFUA SHIRIKA LAKE LA NDEGE

maxresdefault

KAMPALA, UGANDA

SERIKALI ya Uganda imedhamiria kuhakikisha shirika lake la ndege linarejea kutoa huduma za safari za ndege mwaka ujao.

Maofisa wa serikali wameitaja Agosti 2017 kama mwezi ambao Shirika la Ndege la Uganda litaanza kuruka kwa mara nyingine baada ya miaka zaidi ya 16 ya kusimama kwa shughuli zake.

Kwa mujibu wa gazeti la The East African majadiliano baina ya kampuni ya utengenezaji ndege ya Canada, Bombardier na Airbus ya Ufaransa ili kukodi ndege yanaendelea vyema.

“Kufufua shirika la ndege la taifa ni mchakato, hivyo tunatakiwa kuendelea kwa uangalifu na kufuata hatua vizuri, lakini naweza kukuhakikishia kuwa uamuzi ulifanyika na mipango yetu kwa sasa imefikia mahali pazuri. Shirika la Ndege la Uganda litaruka tena mwaka ujao,” Waziri wa Kazi na Usafirishaji, Aggrey Bagiire alisema Alhamisi ya wiki iliyopita.

Vyanzo vya habari vinavyohusiana na suala hilo vinasema mpango wa awali wa serikali ni kukodi ndege sita, nne kwa masafa mafupi ndani ya ukanda na mbili kwa masafa marefu.

Mashirika ya ndege ukanda wa Afrika Mashariki hasa Shirika la Ndege la Kenya, ambalo kwa miaka 15 limetawala kitovu vya usafiri wa ndani na nje ya Uganda, linatarajia kupoteza mapato kutokana na hatua hiyo ya Uganda kufufua shirika lake.

“Tunafuata itifaki na sasa nyaraka zimeshawasilishwa kwa baraza la mawaziri. Mara baraza litakapozipitisha zitawasilishwa Bungeni kupata idhini pamoja na mahitaji ya bajeti. Tumepanga kukodi na kuanza kuruka na mara watu watakapojua tumeanzisha huduma, kisha baada ya kipindi cha miaka miwili, tutanunua ndege yetu wenyewe,” Bagiire alisema.

Aliongeza kuwa ukodishaji ni nafuu, lakini ni kwa kipindi kifupi. “Ni kwa sababu ni ghali kukodi kwa kipindi kirefu, lakini kwa kuanzia ni njia rahisi.”

Mbali ya Kenya, mashirika mengine ya ndege yanayotarajia kuathirika kwa ujio wa Uganda ni yale ya Rwanda, Ethiopia na Afrika Kusini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles