24.6 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

POLISI: MARUFUKU KULIPUA MAFATAKI

9db178_8ccc9ac51e7a480488d7b5c45f2becfe-mv2_d_2048_1365_s_2

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

JESHI la Polisi mkoani Tanga limetangaza vita kali na watu watakaolipua baruti, fataki, eksozi za magari au mlipuko wa aina yoyote wakati wa kipindi cha Sikukuu ya Mwaka Mpya na kusema watakamatwa na kufungwa miaka mitatu jela au faini ya Sh milioni tano.

Hayo yalisemwa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema ni kosa kisheria kumiliki au kufanya kitu chochote kinachoweza kusababisha milipuko au ajali ya moto.

Alisema jambo hilo lipo kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria ya milipuko (Sura ya 45 RE2002), ambapo inatoa adhabu ya faini ya Sh milioni tano au kifungo kisichopungua miaka mitatu au vyote viwili, yaani kifungo na faini kwa pamoja, ikiwa ni fundisho kwa washtakiwa.

“Vilevile sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 RE 2002 kifungu cha 327 na sheria nyingine kama vile sheria za mazingira na sheria zinazohusiana na utunzaji miundombinu mbalimbali zinakataza kuharibu majengo, barabara na mazingira kwa makusudi,” alisema.

“Adhabu zake zinafikia faini inayolingana au kuzidi thamani ya kitu kilichoharibiwa, kifungo cha zaidi ya miaka 14 au vyote wiwili faini na kifungo,” alisema.

Alipiga marufuku watu kuchoma matairi hovyo na kulipua baruti bila kibali, kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Wakati huo huo, Kamanda huyo alisema kipindi cha miezi 11 walifanikiwa kukamata wahamiaji haramu 168, kati yao, 73 ni raia wa Somalia, 85 Waethiopia na 10 ni Wakenya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles