26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

UDSM watengeza mashine kukabili Corona

 MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), waungana na watanzania wote katika kupambana na Virusi vya Corona (Covid-19) hapa nchini kwa kutengeneza mashine ya kutakasa mwili bila kugusa kifaa chochote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 44 ya Biashara, Mvumbuzi wa mashine ya kutakasa mwili, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Alex Malisa alisema kuwa mashine hiyo imebuniwa katika kitengo cha uhandisi Viwanda katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kwaajili ya kupambana na virusi vya Corona vinavyotesa mataifa mengi hapa dunia.

 “Wazo la kuvumbua mashine hii lilikuja kwenye msimu ambao tulikumbwa na janga la Corona, moja ya njia kubuni na kuendeleza mashine ya kutakasa mwili mzima.

“Hii hutumika hata katika hospitali mbalimbali baada ya madaktari kufanya Oparesheni (au Upasuaji) huwa wanajitakasa kama walikuwa wanamfanyia upasuaji mtu ambaye alikuwa anamaradhi yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya hewa kwahiyo wanapita katika mashine hii ili kujitakasa mwili mzima,” alisema Malisa.

Hata hivyo baada ya kuendeleza wazo la kutengeneza mashine hii tukapata ufadhili wa kuitengeneza kutoka kitengo cha uzalishaji uhandisi wa viwanda katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Hii sio mashine ya kwanza kutengeneza ya kwanza tulitengeneza kwaajili ya majaribio pale pale chuo baada ya kuona imefanya kazi vizuri ndio wakatufadhili tena kwaajili ya kutengeneza mashine nyingine,” alisema Malisa.

Alisema kuwa mashine hiyo inagundua yenyewe kama kunamtu na inatoa Sanitaiza ambayo pia imetengenezwa na chuo kikuu cha Dar es Salaam 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles