27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UBINGWA WA VIJANA KUIBEBA SIMBA LIGI KUU

7395f7923335bdef5e8325b8f3c7fd3f

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KATIBU Mkuu wa Klabu ya Simba, Patrick Kahemele, amesema ubingwa walioupata juzi katika mashindano ya ligi ya vijana chini ya miaka 20, umewafungulia njia ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Kikosi cha Simba B kilifanikiwa kunyakua ubingwa baada ya kuifunga Azam FC kwa jumla ya penalti 5-3, katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kwa dakika 120 zilizomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kahemele aliliambia MTANZANIA kuwa, kikosi cha timu ya vijana kimekuwa kikitoa wachezaji wazuri ambao majina yao hupata sifa kubwa kwa baadaye.

“Huu ni mwanzo tu, kwani msimu huu tumejipanga vizuri ili kuhakikisha timu yetu kubwa inatwaa ubingwa wa ligi kuu, Kombe la FA na Kombe la Mapinduzi,” alisema.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa timu ya Azam, Iddy Nassor, alisema wachezaji wake walijitahidi kucheza soka safi hadi kufanikiwa kuingia hatua ya fainali, ingawa walishindwa kutwaa ubingwa.

“Pamoja na wachezaji wetu kucheza kwa muda mrefu bila kupata muda wa kupumzika, lakini walijitahidi kupambana kuwania kutwaa ubingwa, ingawa bahati haikuwa upande wetu.

“Hata hivyo, tuliwakosa wachezaji wetu muhimu ambao walikuwa kwenye timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kutokana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuzuia kadi zao,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles