*Kikwete ampongeza, amtaka acheze Ulaya
NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM
UBALOZI wa Ubelgiji nchini jana ulimpa viza mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani,
Mbwana Samatta, ili kujiunga na timu yake mpya ya K.R.C Genk, huku ikimtakia mafanikio mema katika masuala yake.
Samatta alitwaa tuzo hiyo usiku wa Alhamisi ya wiki iliyopita na kupewa dola za Kimarekani15,000 (sawa na shilingi milioni 32 za Tanzania), baada ya kuwashinda wenzake wawili Mualgeria, Baghdad Boundjah, anayekipiga katika
klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia na kipa machachari wa TP Mazembe ya Congo DR, Robert Kidiaba.
Nyota huyo Mtanzania aliisaidia timu yake ya TP Mazembe kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika, huku akiibuka mfungaji bora baada ya kufikisha mabao saba na sasa anatarajia kujiunga na Klabu ya K.R.C ya Genk kwa mkataba wa miaka miwili na nusu ukiwa na thamani ya dola za Kimarekani 550,000 sawa na shilingi bilioni 1 za Tanzania.
Chanzo cha habari karibu na Samatta kilithibitisha mchezaji huyo kupewa viza jana, huku ubalozi wa nchi hiyo ukimpa baraka ya kufanikiwa katika mazungumzo na timu hiyo.
“Suala la visa halikuwa nawasiwasi kabisa kwa Samatta, ndiyo maana haikuchukua muda mrefu kufanikisha,” kilisema