25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Twiga Bancorp kupata wawekezaji wapya

pictwigabanc

Na JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

SIKU 10 baada ya Benki ya Twiga Bancorp Ltd kutangazwa kufilisika, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema ipo katika mchakato wa kutafuta wawekezaji wapya watakaotoa mtaji kwa benki hiyo huku ikiwaondoa hofu watu walioweka amana katika benki nyingine.

Oktoba 28 mwaka huu Benki ya Twiga ilifungwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa BoT ili kufanya tathmini ya hali ya fedha ya benki hiyo ambayo inaelezwa kuwa na hasara ya zaidi ya Sh bilioni 20.

Taarifa   iliyotolewa na BoT jana ilisema njia ya kutafuta wawekezaji wapya ndiyo inayopewa kipaumbele katika mchakato wa kutafuta mbadala wa kutatua tatizo la mtaji linaloikabili benki hiyo.

“Benki Kuu ipo katika mchakato wa kupitia na kuchambua njia mbadala za kutatua tatizo la mtaji linaloikabili Twiga Bancorp.

“Njia inayopewa kipaumbele ni kutafuta mtaji kutoka kwa wawekezaji wapya, mchakato utakaowahitaji kuchambua hali halisi ya taarifa za hesabu za Twiga (due diligence).

“Hatua hii inatarajiwa kuchukua takriban wiki tatu na itakapokamilika, Benki Kuu itaingia makubaliano na wawekezaji wapya kuhakikisha wanaingiza mtaji unaohitajika haraka iwezekanavyo shughuli za kawaida za kibenki ziweze kuendelea,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza:

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika benki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.”

Katika hatua nyingine, BoT imekamilisha hatua ya kutathmini hali ya fedha ya Benki ya Twiga na    kuanzia kesho itaanza kutoa baadhi ya huduma ikiwamo kupokea marejesho ya mikopo wakati mchakato wa kuwatafuta wawekezaji wapya ukiendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles