25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tuzo za Oscar zamliza Leonardo DiCaprio

leonardo-dicaprio-inline-zoom-e780bd67-8bfe-4cb1-a724-88c8403b9bbaBADI MCHOMOLO NA MITANDAO

TUZO za Oscar kwa mwaka 2016 zimetolewa juzi katika jiji la Los Angeles, nchini Marekani, huku wasanii mbalimbali wakijinyakulia tuzo hizo zilizotimiza mara ya 88 tangu kuanzishwa kwake.

Vipengele 24 viliwaniwa na wasanii katika tuzo hizo zinazohusisha filamu zinazofanya vizuri katika chati ya Billboard na maeneo mengine duniani.

Filamu ya ‘The Revenant’ iliyoleta ushindani mkubwa katika anga la filamu duniani imefanikiwa kutwaa tuzo tatu kati ya vipengele 10 ilivyokuwa ikishindania.

Filamu ya ‘The Revenant’ iliachiwa mwaka jana Desemba 25, ambapo ilisifiwa sana kutokana na kuongozwa vyema, kuwa na washiriki wa kiwango cha juu na walioitumia vyema nafasi ya uhusika wao na pia ilisifika kwa kuwa na mfumo bora wa sauti na rangi zilizotumiwa.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yalijiri katika utoaji wa tuzo hizo ambapo hafla hiyo ilitumia saa 3:37.

Leonardo DiCaprio atoa chozi jukwaani

Bila kutarajia, mwigizaji aliyetamba katika filamu mbalimbali, zikiwemo ‘The Revenant’ na ‘Titanic’, Leonardo DiCaprio, alijikuta akiangusha chozi la furaha kwa kuibuka mwigizaji bora wa kiume katika tuzo hizo.

Hiyo ilikuwa tuzo ya kwanza kubwa kwake mbele ya idadi kubwa ya mashabiki.

“Tuzo hii siyo ya peke yangu, ninaamini watu wote wameonyesha ushirikiano katika maisha yangu ya filamu, kwa ushauri na kunisimamia katika filamu hiyo, asanteni sana,” alisema DiCaprio.

Wapinzani wake katika kinyang’anyiro hicho walikuwa Bryan Cranston aliyecheza filamu ya Trumbo, Matt Damon ‘The Martian’, Michael Fassbender ‘Steve Jobs’ na Eddie Redmayne ‘The Danish Girl’.

Filamu bora zaidi

Kulikuwa na filamu nane zilizokuwa zikiwania tuzo hizo, ambazo ni ‘Spotlight’, ‘The Big Short’, ‘Bridge of Spies’, ‘Brooklyn’, ‘Mad Max ‘Fury Road’, ‘The Martian’, ‘The Revenant’ na ‘Room’ ambapo ‘Spotlight’ iliibuka filamu bora ya mwaka.

Lakini kwenye mitandao mingi ya kijamii kumeonekana kuwa na maneno kwamba haikuwa filamu bora zaidi, huku wengi wakidai kwamba filamu ya ‘Mad Max’ ndiyo ilistahili kutwaa tuzo hiyo.

Mwigizaji bora wa kike

Brie Larson, ambaye alicheza filamu ya ‘Room’, ndiye aliyefanikiwa kuwa mwigizaji bora wa kike, akiwabwaga Cate Blanchett, Jennifer Lawrence, Charlotte Rampling na Saoirse Ronan.

Mwongozaji bora wa filamu

Mwigizaji bora wa kiume alitoka katika filamu ya ‘The Revenant’ iliyofanikiwa kutwaa tuzo nyingine mbili, ikiwemo mwongozaji bora, ikifuatiwa na filamu ya Mad Max ambayo nayo imefanya vizuri katika tuzo hizo.

Mwongozaji bora wa tuzo hizo, Alejandro G Inarritu pia alitokana na filamu ya ‘The Revenant’, akiwa anashindana na Lenny Abrahamson aliyeongoza filamu ya ‘Room’, Tom McCarthy aliyeongoza filamu ya ‘Spotlight’, Adam McKay wa ‘The Big Short’ na George Miller wa filamu ya ‘Mad Max’.

Kabla ya tuzo

Mwezi mmoja kabla ya tuzo hizo kutangazwa kulikuwa na malalamiko kwa baadhi ya wasanii wa filamu na wadau mbalimbali kwa madai kwamba kumefanyika ubaguzi wa rangi, kutokana na nafasi kubwa ya watu weusi kupewa nafasi ya utoaji wa tuzo badala ya ushiriki na upokeaji wa tuzo hizo.

Mitandao ya kijamii

Kupitia mitandao ya kijamii, tuzo hizo zimejishushia heshima kutokana na ubaguzi wa rangi unaoendelea kwa kuwapa nafasi watu weupe na kuacha watu weusi wenye uwezo mkubwa.

Sinema bora

The Revenant’ iliibuka Sinema bora dhidi ya Carol, The Hateful Eight, Mad Max: Fury Road na Sicario. Mbali na hizo kulikuwa na tuzo nyingine mbalimbali.

Tuzo nyingine

Tuzo nyingine zilizotolewa ni pamoja na filamu bora ya lugha ya kigeni, ‘Son of Saul’ – Hungary. Filamu fupi bora ya katuni hai ‘Bear Story (Gabriel Osorio na Pato Escala), ‘Prologue Sanjay Super Team’, ‘We Can’t Live without Cosmos’ na ‘World of Tomorrow’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles