Na Clara Matimo, Mwanza
 “Tutahakikisha tunaondoa vikwazo vyote mlivyonavyo wafanyabiashara ili
mfanye biashara katika mazingira mazuri, rushwa hainanafasi ndani ya mkoa
 huu, usitoe rushwa kwa mtumishi wa umma ili akutatulie changamoto yoyote
uliyonayo, fanyeni biashara zenu kwa uhuru lipeni kodi zinazostahili kwa
mujibu wa sheria na taratibu, kiu yangu ni kuona kikao hiki kinatuletea
tija kwa kuinua uchumi wa mkoa wetu.
“Ushauri wangu kwenu, kumbukeni kumtolea Mungu fungu la kumi(zaka)Â na
sadaka ili abariki biashara zenu pia toeni kwenye huduma inayogusa jamii
kama zahanati na shule hakika Mungu atabariki na kulinda biashara
zenu,”amesema Gabriel Kenene.
Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye viwanda na Kilimo
Tanzania(TCCIA) Mkoa wa Mwanza, Gabriel Kenene, alisema miongoni mwa
changamoto za mazingira ya biashara wanazokabiliana nazo ni pamoja na
serikali kuchelewesha malipo kwa wazabuni na wakandarasi hivyo kusababisha
wahusika kulipa riba kubwa katika mabenki hali inayopunguza uwezo wao wa
kuchangia uchumi wa nchi.
“Tunaomba sheria zirekebishwe ziendane na hali halisi ya biashara zilivyo
sasa, hasa kwa wakandarasi ambao wateja wao wakubwa ni serikali maana
wanajikuta wanalipishwa faini, riba na withholding tax baada ya wao
kuchelewa kulipwa na serikali,” alisema Kenene.
Kwa upande wake Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania ( TIC) Kanda ya
Ziwa, Pendo Gondwe, alipongeza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuzitaka
halmashuri kutenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji maana itasaidia
kuhamasisha na kuongeza wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo,
utalii na uvuvi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania(Tafu), Bakari Kadabi, aliiomba
serikali kupunguza kodi ya zuio ya asilimia mbili kila wanapouza bidhaa
zao walau hadi asilimia 0.5Â iliyotokana na mabadiliko ya sheria ya
usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 kifungu cha 22 sura ya 438Â yaliyofanywa
Juni 30 yakitokea kwenye sheria ya fedha ya mwaka 2021 ambayo yameanza
kutukika Julai Mosi mwaka huu kwa kuwa gharama za uendeshaji ni kubwa hivyo
tozo hiyo ni kikwazo kwao.