25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

Pacquiao kugombea urais

STAA wa ndondi duniani, Manny Pacquiao, ametangaza nia ya kuwania kiti cha urais katika Uchaguzi ujao wa Ufilipino unaotarajiwa kufanyikwa mwakani.

Pacquiao, ambaye kwa sasa ni seneta nchini humo, ameingia kwenye kinyang’anyiro baada ya kuteuliwa na Chama tawala, PDP-Laban.

“Mimi ni mpambanaji na nitakuwa mpambanaji ndani na nje ya ulingo,” amesema Pacquiao mwenye umri wa miaka 42.

Katika hotuba yake, mwanamasumbwi huyo ameahidi kuunda Serikali yenye kujali masilahi ya raia wa Ufilipino, pia akidai itapambwa na uwazi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,953FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles