26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

“Tumieni taaluma zenu kuleta majibu ya changamoto”- Serikali

Na Mwandishi Wetu

Serikali imezitaka Taasisi za Utafiti wa masuala ya Ukimwi kuja na suluhisho la changamoto zinzokwamisha Tanzania kushindwa kufikia malengo kwenye tisini tatu ikiwamo kuiwezesha Tanzania kujitegemea yenyewe badala ya kusubiri wahusani.

Hayo yalielezwa juzi, na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof Mabula Mchembe wakati alipokuwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la kisayansi la masuala ya Ukimwi lililofanyika mkoani Kilimanjaro.

Alisema ni wakati wa wataalamu mbalimbali kutumia utaalam wao katika kuiwezesha nchi kujitegemea yenyewe katika upatikanaji wa dawa na fedha za kutekeleza afua mbalimbali za Ukimwi badala ya kuwategemea wahisani.

“Tafiti zetu zinatakiwa zituelekeze kwenye suluhisho la changamoto zinazotukwamisha katika kufikia tisini tatu badala ya kuwategemea wahisani wataalamu wetu watusaidie ili tuweze kusimama wenyewe, tuweze kutengeneza dawa zetu kwa bahati nzuri Tanzania tumebarikiwa miti mingi inayofaa kutumika kwa ajili ya tiba za mitishamba kama artemisia badala ya kuwategemea wahisani,”alisema Prof Mchembe.

Alisema maadhimisho ya mwaka huu ambayo yanabebwa na kauli mbiu ya “Mshikamano wa Kimataifa-Tuwajibike kwa Pamoja” inamtaka kila mtu kuwajibika kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia na jamii kwa ujumla kudhibiti maambukizi mapya ya VVU, hivyo kila mtu awajibike.

“TACAIDS katika maadhimisho haya kwa juma zima watakuwa wanatoa tathmini ya mwelekeo wa kitaifa wa mwitikio wa VVU na UKIMWI, elimu na taarifa muhimu zihusuyo mwitikio wa VVU na Ukimwi vitatolewa bure wananchi wote wa Kilimanjaro tumieni fursa hii tuwajibike kwa pamoja,” alisema Prof Mchembe.

Akizungumzia Mfuko wa Udhamini wa Udhibiti Ukimwi (ATF) alisema pamoja na serikali kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi(TACAIDS) zimekuwa zikiwahamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuuwezesha mfuko ambapo fedha zinazopatikana zinatumika katika kuwezesha shughuli za VVU na Ukimwi lakini bado inahitajika utafiti wa kuutunisha mfuko huo ili uweze kuboresha huduma zake.

“Tumieni fursa hii adhimu katika kongamano hili kwa kutafakari namna bora ya kutekeleza afua zitakazowezesha kudhibiti maambukizi mapya ya VVU kwa kutoa mawazo chanya ya nini kifanyike ili tuweze kusonga mbele, hapa kuna wanasayansi wataalamu wengi kutoka Taasisi za Umma na wadau mbalimbali wa masuala ya Ukimwi tupatieni majibu ya nini tufanye ili tuweze kufikia azimio la sifuri tatu ifikapo mwaka 2030,” alisema Prof Mchembe.

Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wahisani na wadau mbalimbali wa wanaotekeleza shughuli za Mwitikio wa Ukimwi kama Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu (Global Fund), PEPFAR, UN na Taasisi za hapa nchini ikimwamo TACAIDS, NACP na TAMISEMI, kwa michango yao katika kudhibiti maambukizi mapya ya VVU sambamba na kuhakikisha matumizi sahihi na endelevu kwa WAVIU zinapatikana bure nchi nzima.

Akizungumzia hali ya maambukizi ya VVU Kwa Mkoa wa Kilimanjaro, Mratibu wa mkoa huo wa Ukimwi Dk. Eligius Mosile alisema kuwa Mkoa huo maambukizi mapya ya VVU yamekuwa yakipungua kutokana na ushirikiano mzuri baina ya uongozi wa Mkoa na wadau mbalimbali katika kutekeleza afua za Ukimwi mkoani hapo.

“Ukiangalia tafiti za hali ya maambukizi ya VVU THIS katika awamu zote nne kama mkoa tumekuwa tukifanya vizuri ambapo matokeo ya tafiti kwa mwaka 2003/2004 maambukizi yalikuwa asilimia 7.3 tafiti zilizofuata mwaka 2007/2008 yalikuwa ni asilimia 1.9%, tafiti za mwaka 2011/2012 ni asilimia 3.8 na tafiti za mwisho mwa mwaka 2016/2017 yalikuwa ni asilimia 2.6,”alisema Dk. Mosile.

Aliwataka wakazi wa Kilimanjaro na mikoa jirani kufika uwanja wa Mandale kupata huduma bila malipo kutoka kwa wataalamu wa afya ya upimaji wa VVU, uchunguzi wa magonjwa sugu kama kisukari, saratani ya shingo ya kizazi, pamoja na uchangiaji damu kwa muda wa wiki nzima ya Maadhimisho haya yanayofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mandela Kata ya Pasua Manispaa ya Moshi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles