24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

“Tumieni mashine ya kisasaa kupima madini”- TMDA

Aveline Kitomary, Mwanza

Mamlaka ya Dawa, vifaa tiba na vitendanishi (TMDA) Kanda ya Ziwa imewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kupima sampuli zao kutokana na uwepo wa mashine yenye uwezo mkubwa wa kupima madini katika maabara ya kanda hiyo.

Mashine hiyo ya Micro Plasma Atomic Emission Spectrophotometer (MPAES) inauwezo wa kupima madini mbalimbali yakiwemo tembo, copper, zink, mecyur na zingine.

Akizungumza wakati wa ziara ya Waandishi wa Habari, Kaimu Mkuu wa Maabara hiyo, Busugu Nyamweri amesema ni muhimu wadau mbalimbali kutumia mashine hiyo katika kufanya tafiti mbalimbali.

“Kwasasa vifaa vipo na kama kuna taasisi inahitaji kufanya tafiti katika eneo hilo uwezekano huo upo na wanakaribishwa kufanya tafiti lengo letu ni kupanua wigo wa upimaji sampuli kwa wadau mbalimbali katika eneo la kanda ya ziwa.

“Hasa kuangazia vitu vinayoathiri afya za watu hivyo tunakaribisha taasisi za tafiti kuleta sampuli zao katika maabara hii tuweze kupima na tunawakaribisha wadau, taasisi za afya kama NIMR, zingine binafsi wajue kuwa TMDA ina hivi vifaa,”amasema Nyamweri.

Mtaalamu wa Maabara, Jovinary Rwezahura akieleza namna mashine hiyo inavyofanyakazi

Kwa upande wake, Mtaalamu wa Maabara, Jovinary Rwezahura, amesema mashine ya MPAES inauwezo mkubwa wakupima madini zaidi ya moja kwa mara moja.

“Hii mashine kama zilivyo mashine zingine zinatumika  kupima madini (heavy metal)  tunasema madini tembo na zingine kama   kupima sodium,copper, zink, meckyur na mashine  hiyo inauwezo mkubwa hasa katika  kupima madini mengi kwa wakati mmoja  lakini mashine zingine haziwezi kufanya kazi zote hizo kwa wakati moja,”ameeleza Rwazehura.

Amesema upekee mwingine wa mashine ya MPAES ni matumizi ya gesi ya Nitrogen ambayo inajikusanya kutoka katika mazingira.  

“Faida nyingine hatutumii gesi zingine kama petroleum gesi ambazo hauruhusiwi kuacha mpaka uhakikishe imezimwa  kama gesi zinazotumika majumbani lakini hii kwa sababu ya Nitrogen naweza kuwasha na kuweka sampuli na nikaendelea kufanya kazi zingine, baadae naweza kuizima.

“Mashine hii inatumika kupima madini kwenye vifaa tiba, maji, vipodozi, vyakula, sukari, mchicha pia tunapima madini hata kwenye maji pia tunaangali madini ambayo hayaruhusiwi kuwepo kama madini tembo kwa kiasi inayohitajika lakini hayaruhusiwi kuwepo na kama yapo kuna kiasi kinaangaliwa.

“Madini tembo hayahitajiki yanaweza kuharibu figo, mifupa inaweza isiwe imara, madini ya mekyuri yanaweza kuathiri mifumo ya neva ukawa unasahau kwahiyo madini tembo hayahitaji kabisa lakini tunaangali kama kuna kiwango kidogo ambacho kinaweza kuvumilka,”amebainisha Rwezahura.

Aidha, amefafanua kuwa, huwa wanapima pia vipodozi kwani vikiwa na madini tembo ngozi itaharibika na kuongeza kuwa mashine hiyo inatumika kupima vifaa tiba kama sindano.

“Katika upimaji hatuweki sindano moja kwa moja kuna taratibu za kufanya kwa mfano madini yaliyoko kwenye sindano, tunachukua sindano tunaweka kwenye maji kwa muda fulani kama madini tembo yapo yanatakuwa yanatoka yanaingia kwenye maji.

“Kisha yale maji tunayachukua na kuja kupima kwenye mashine hivyo kama yapo tutayaona kama hayapo pia tutajua,”amesema Rwezahura.

Ameongeza “Kama mtu akileta tukapima kama tunazuia  tunamueleza kuwa tumezui  kutokana na sababu zilizopo na huwa tunaangali viwango vya kimataifa na tunaangali kama kiwango kimepungu au kimezidi na kama kinavumilika,” amehitimisha Rwezahura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles