23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TMDA Mwanza kuwa maabara bora Afrika upimaji vipukusi

Aveline Kitomary, Mwanza

Mamlaka ya Dawa, vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA) Kanda ya Ziwa imejipanga kuhakikisha inakuwa maabara bora barani Afrika na yenye kukidhi viwango vya Shirika la Afya Duniani(WHO) katika upimaji wa vipukusi.

Mpango mkakati huo umebainishwa na Kaimu Meneja wa TMDA, Sophia Mziray, ambapo amesema kuwa mabaara hiyo ya ukanda wa ziwa inatarajiwa kuwa bora na bobezi kwa kupima vipukusi barani Afrika.

Mziray amesema maabara hiyo itabobea katika upimaji wa vipukusi kama vile vitakasa mikono, detto, sprit na zingine ambazo zinatumika nje ya mwili.

Kaimu Meneja wa TMDA, Sophia Mziray

Akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari katika maabara hiyo jijini Mwanza, Mziray amesma maabara hiyo itakuwa na vifaa vyote vinavyohitajika na itakuwa na wataalam wabobezi.

“Tunataka kuifanya maabara hii kuwa kubwa na bora Afrika, hiyo itaenda sambamba na kuifanya kuwa ya kisasa na bobezi ya kuweza kuchunguza vipukusi kwahiyo tuko kwenye hatua mbalimbali ya kuandaa wachunguzi wetu waweze kuwa wabobezi lakini vilevile na kuandaa mahitaji ya kulifanikisha hilo,” amesema Mziray.

Amesema katika kuelekea hatua za ubobezi wameanza kuanda wataalamu kuwa wabobezi.

“Tunaangali tunahitaji nini ili kuwa bora tunahitaji document tumeziandaa vizuri ambazo zinaweza kutusaidia na kama vifaa tunaagali je vinajitosheleza, lakini unaanga kama rasilimali tulizonazo zinajitosheleza hivyo tunata kuwa maabara inayotambulika na Shirika la Afya Duniani (WHO) ili maabara iweze kukubalika duniani kwa document.

“Kwa kawaida WHO huwa wanachunguza maabara kwa kufanya kaguzi mbalimbali ikiwemo kuangalia wataalmu kama wanaubobezi na mwaka huu tutaanza ukaguzi wa kwanza tunataka viwango vya kimataifa za kuwa maabara bora za kufanya uchunguzi,”amefafanua Mziray.

Ameeleza kuwa maabara hii bado inachunguza dawa kwa eneo la mipaka ya kanda ya ziwa na kutoka katika kanda zingine ambazo pia TMDA inaofisi ili kusadia maabara kubwa ya TMDA iliyoko jijini Dar es Salaam.

“Lakini pia tunafanya udhibiti kati mikoa mbalimbali ikiwemo Sirari, Kyelwa huu unaingia Uganda lakini haujapitishwa kusimamia sisi, tuna bandari ya Mwanza South, Uwanja wa ndege wa Mwanza.

“Tunashirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya afya na wadau katika halmashauri hawa ni wadau katika kudhibiti bidhaa za dawa, vifaa tiba pamoja na vitendanishi,”amebainisha Mziray.

Amesema pia wanatoa elimu kwa jamii ili waweze kugundua kama bidhaa ni salama na inaubora, ufanisi na usalama.

“Lengo letu ni kuhakikisha watanzania wanapata bidhaa bora na zenye ufanisi hivyo tunawaelimisha kuwa ni jukumu lao kuwa na wenyewe ni wadhibiti kwahiyo wakiwa wanaona bidhaa hizo waweze kuzichunguza na kuangalia bidhaa ambazo ni duni na watu taarifa na sisi tunafanyiakazi.

“Kwa vile tunasimamia kuingia nchini udhibiti tunaoongelea ni kufuatilia sokoni kuhakikisha kwamba zinaendelea kuwa na ubora ule ule na ufanisi wa wakati wa usajili, tunaingia kwenye soko na tunachukua sampuli tunaangalia je inakidhi vigezo na ubora uleule,”amesema.

Ameeleza pia wanafanya ufatilia wa madhara ya dawa kwa jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya.

“Tunafahamu kuwa dawa ni kemikali kuna madhara yanayojulikana na yale yasiyojulika na yale yanayojulikana utakuta yameorodheshwa kwenye karatasi (package insert).

“Lakini hata hayo madhara ukisoma yakaonekana  yanazidi kiwango kisichotarajiwa unatoa taarifa kwetu  kwahiyo tuna mfumo mzuri kwa watumiajia, tunashirikana na Wizara ya Afya wakiwemo madakari, wafamasia na manesi kama watabaini wagonjwa aliopata madhara wanatuambia kisha wanatuingizia taarifa na kuchukua hatua, lakini hata mgonjwa mwenyewe anaweza kututumia taarifa moja kwa  moja,”ameeleza.

Amesema wanashirikiana na watumishi wa afya walioko katika halmashauri ili kufanikisha zoezi la kudhibiti soko la vifaa tiba na vitendashi.

“Lengo la Mamlaka ni kulinda afya ya jamii na kuwa na uhakika wa vifaa na dawa wanazotumia. Pia maabara hizi tunatumia kwa faida kwani tunapata fedha za kigeni ambazo zinaongeza pato la taifa kwani nchi mbalimbali wanakuja kupima sampuli zao katika maabara yetu ,”ameeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles