24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

“Tumieni mahubiri yenu kusaidia mapambano dhidi ya UKIMWI”

Na Faraja Masinde, Mbeya

Viongozi wa Dini nchini wametakiwa kutumia majukwaa yao katika kusaidia Mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI ikiwamo kutoa elimu sahihi badala ya kushawishi Waviu kuacha dawa.

Wito huo umetolewa leo jijini Mbeya na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk. Vicent Anney, wakati akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Juma Homera kwenye Mdahalo wa Viongozi wa Dini na Vijana kuhusu UKIMWI.

Baadhi ya washiriki wa Mdahalo huo wakifuatilia mada mbalimbali.

Amesema Viongozi hao kwa wakati mwingine wamekuwa ni sababu ya watu wanaoishi na VVU kuacha kutumia dawa kwa kuamia kuwa wanaweza kupona kanisani.

“Viongozi wa Dini ni watu mnaoaminiwa sana na Jamii, hivyo hamna budi kutumia majukwaa yenu ya dini kwa ajili ya kutoa Elimu sahihi ya UKIMWI badala ya kuwaeleza waumini kuwa wanaweza kupona kwa maombi.

“Kwani hakuna mahala kwenye Biblia au Msaafu ambapo pame andikwa kuwa kutumia dawa ni dhambi, hivyo tumieni vituo vyenu vya Televisheni mtandao kwa ajili ya kujenga mtazamo chanya wa matumizi ya dawa za ARVs kwa Waviu na si kuwambia waache dawa,” amesema Dk. Anney.

Ameongeza kuwa kama ambavyo Viongozi wa Dini hawakatazi waumini wao kutumia dawa za Malaria basi wanapaswa kufanya hivyo pia kwenye ARVs na Chanjo ya Uviko- 19.

Mdahalo unaendelea…

Mdahalo huo ulioandaliwa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) unaoendelea ukihusisha Viongozi wa Dini na Vijana ambao ni sehemu ya Maadhimisho ya UKIMWI duniani ambayo Kitaifa yatafanyika jijini Mbeya Desemba Mosi yakiwa na Kauli mbiu ya “Zingatia Usawa, Tokomeza UKIMWI, Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, yatakayiifanyika katika viwanja vya Ruandanzovwe.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko, alisema lengo la mdahalo huo ni kujadili mchango wa Viongozi wa Dini katika mwitikio wa VVU na UKIMWI nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles