24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mashirika ya Kigeni yazidi kuvutiwa kuwekeza katika sekta ya nishati nchini

Na Dorina Makaya,Dar-es-Salaam

Idadi ya mashirika ya kigeni yanayovutiwa kuwekeza katika sekta ya Nishati nchini yameendelea kuongezeka ikiwemo katika sekta ndogo ya umeme na nishati Jadidifu.

Waziri wa Nishati, January Makamba, leo Novemba 29, 2021, amekutana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mitsubishi iliyopo jijini Dar es Salaam, Kenji Nishizaki na kujadili masuala ya ushirikiano wa kisekta na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.

Miongoni mwa masuala waliyoyazungumzia katika mkutano huo, uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Nishati, ni pamoja na kupanua wigo wa biashara kwa kutazama fursa zilizopo za uwekezaji katika maeneo ya sekta ndogo ya umeme, mafuta na gesi asilia pamoja na ushirikiano wa kisekta kwa ujumla na serikali ya Tanzania

Waziri Makamba, amewakaribisha Kampuni ya Mitsubishi kwa ajili ya kuwekeza hapa nchini na ameelekeza mashirika ya TPDC na TANESCO kutazama kwa upana zaidi wigo huo wa uwekezaji ambao Mitsubishi wanataka kuwekeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles