Na Shermarx Ngahemera
ALIYEWAHI kuwa Balozi wa Canada nchini Tanzania, Andrew McAlister, anajitahidi kupigania mkataba wa madini kutoka kwa Barrick Corporation uende kwa
Kampuni Jervois Mining Limited ya Australia.
Mapambano ya McAlister yamejumuisha vile vile timu ya magwiji wa madini na washauri ili kuweza kulipata eneo la Kabanga Nickel katika Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, baada ya Tume ya Madini kufuta umiliki wa Barrick.
McAlister anaongoza timu hiyo mahiri ili kusaidia kukabiliana na Shirika la Barrick Gold la mradi wa madini ya Nickel yenye faida kubwa duniani eneo ambalo umetamkwa kama mojawapo ya amana kubwa zaidi ya nickel-cobalt duniani kote.
Kazi ya timu hiyo ni kuifanya Serikali ya Tanzania ifanye maamuzi ya kudumu kuinyang’anya Kampuni ya Barrick Gold kwani kwa mtazamo wa Jervois Mining eneo hilo ni bora na muhimu kwa kampuni yake kama italipata ili kuweza kuvuna hazina hiyo ambayo iko tayari, inasemekana ni ya pili kwa ukubwa duniani na ina kiwango cha mavuno kikubwa ya asilimia 2.8.
Hatua hiyo ya kunyang’anyana inakuja baada ya Serikali kupitia Tume ya Madini kufuta leseni ya uhifadhi amana (retention licence) kwa ajili ya mradi wa Kabanga isiyo na maendeleo mwezi Mei mwaka huu ikiwa kama sehemu ya utekelezaji wa utawala mpya wa madini nchini.
Serikali hapo awali ilitoa leseni ya uhifadhi kwa wenye wamiliki wa leseni ya Utafutaji (exploration) ya baada ya kutambua kwenye maeneo yao au jirani kuwa kuna amana ya madini (mineral deposit) ndani ya eneo ambalo linaweza kuwa na umuhimu wa biashara lakini haiwezi kuendelezwa mara moja kwa sababu ya vikwazo vya kiufundi, hali mbaya ya soko au mambo mengine ya kiuchumi. Eneo kama hilo liliwekwa kiporo ili liendelezwe baadaye na mhusika hali ikiwa inaruhusu na hivyo kwa kiasi fulani kuzuia ushindani wa uendelezaji maeneo yenye madini.
Sheria mpya yafuta ukiritimba
Lakini chini ya sheria mpya za madini ambayo ilipitishwa na Bunge mwezi Julai mwaka jana, 2017, leseni zote za kuhifadhiwa (retention) zilifutwa kwa ufanisi, kwa maana Barrick Gold Corp na Glencore Plc, ambao walimiliki kwa pamoja mradi wa ubia wa nickel 50-50 wa Kabanga, waliondolewa haki zao kwa utajiri wa madini amana.
Katika kikao chake cha kwanza cha utendaji kazi,
Tume ya Madini ilifuta leseni zote 11 za kuhodhi maeneo ya uchimbaji madini na maeneo hayo yamerudishwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena wale wa mwanzo.
Vile vile ilifungua rasmi uombaji na utoaji wa leseni za biashara (Mineral Trading license) na udalali wa madini (Broker’s License) na wachimbaji wadogo (Primary License) mwezi uliopita.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, alisema hatua hiyo imefikiwa kwenye kikao cha kwanza cha tume hiyo kilichofanyika Aprili 30, mwaka huu.
Alisema leseni hizo zimefutwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ikisomwa pamoja na marekebisho ya mwaka 2017 na kanuni ya 21 ya kanuni za madini (Haki Madini) ya mwaka 2018.
Alitoa maelezo ya kina juu ya sababu za kuchukua hatua hizo kali.
“Ukiangalia kwa undani kabisa utakuta wenye leseni walikuwa hawachimbi, mfano wa wachimbaji wa madini ya Nickel walikuwa wakiona bei imeshuka eneo hili wanaliacha na hujui zitakuja kupanda lini, hivyo eneo linakuwa chini ya mamlaka ya mtu ambaye halitumii, na haliendelezi. Hivyo tumefuta kwa msingi wa sheria,” alisema.
Alitaja kampuni zilizofutiwa kuwa ni Kabanga Nickel Company Ltd (Kagera), Nachingwea Nickel Ltd (Lindi) na Precious Metal Refinery Company Ltd (Simiyu) zilizopewa kuchimba madini ya Nickel lakini walichofanya ni kuhodhi maeneo tu.
Kwa madini ya dhahabu ni National Mineral Development Corporation Limited (Shinyanga), Mabangu Mining Ltd na Resolute (Tanzania) Ltd ya Geita kutoka ukanda wa ziwa.
Kampuni ya Bafex Tanzania Ltd iliyokuwa na migodi minne ya dhahabu, shaba na almasi (Mbeya) na kampuni ya Wigu Hill Mining Company Ltd (Morogoro) iliyokuwa na eneo la uchimbaji wa madini ya Rare Earth elements (REE).
Ufutaji leseni hizo kimsingi inaiwezesha serikali kuyatoa tean kwa wawekezaji wapya kwa bei na masharti mapya ikiwamo kupata haki mahsusi (carrier rights) ya asilimia 16 ya mgodi bilagharama ili iwe mshiriki na mwenye hisa kwenye mgodi.
“Tume imeazimia kuimarisha usimamizi wa Sheria ya madini kwa lengo la kuhakikisha Serikali inamiliki hisa zisizopungua asilimia 16 ya mtaji wa kampuni bure kwa migodi ya kati na mikubwa,” alisema Kikula na kuongeza: “Ili kuhakikisha wazawa wanashirikishwa ipasavyo katika miradi ya madini na kunufaisha jamii katika maeneo ya migodi na taifa kwa ujumla,” alisema.
Utoaji wa leseni
Profesa Kikula aliwataka waombaji leseni za madini kukamilisha maombi yao ili yaendane na matakwa ya mapya ya Sheria ya Madini na kukumbushia kuwa hadi kufikia Julai 4 mwaka jana, kulikuwa na jumla ya maombi mapya ya leseni za uchimbaji wa kati zipatazo 15 na kuhuisha leseni 21.
Profesa Kikula alisema maombi ya leseni za uchimbaji mdogo yalikuwa ni 4,345 katika ofisi za madini za mikoa na wilaya kote nchini na maombi 240 ya leseni za utafutaji wa madini na kati ya maombi hayo 86 yalishalipiwa ada ya kuandalia leseni.
“Waombaji wote wa leseni za madini wanatakiwa kukamilisha maombi yao ili yaendane na matakwa ya Sheria ya Madini,” alisisitiza.
Profesa Kikula alisema kwa waombaji wa leseni za uchimbaji wa kati na mkubwa wanatakiwa kuwasilisha vilevile andiko la Mpango kazi na Mpango wa namna ya kuwashirikisha Watanzania katika uchimbaji wa madini na Mpango wa namna watakavyosaidia wananchi wanaozunguka mgodi ili uwe msingi wa makubaliano ya utendaji kazi kwa eneo husika.
Kiapo cha uadilifu
Mwenyekiti wa Tume ya Madini pia aliwataka waombaji kujua wanatakiwa kuwasilisha kiapo cha uadilifu, ili kama mtu atafanya mambo ambayo hayana uadilifu sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Alisema kwa waombaji wa leseni za utafutaji wa madini wanatakiwa kuwasilisha taarifa za vitendea kazi na taarifa rasmi za hesabu zilizokaguliwa na mhasibu anayeaminika (approved accountant).
Isitoshe Profesa Kikula alisema kwa waombaji wa leseni za uchimbaji wa kati na mkubwa aliwataka kuwasilisha cheti cha tathmini ya Athari za Mazingira, taarifa za upembuzi yakinifu, vitendea kazi, hesabu zilizokaguliwa na uthibitisho wa kulipa tathmini ya fidia.
Alisisitiza kuwa Uthibitisho wa tathmini ya fidia ni jambo la muhimu kwani migogoro mingi ya madini inatokana na hayo, pia wananchi kutopewa elimu kamili juu ya nini kinakuja na wao wanapata faida gani na ndiyo hayo mambo tatat ambayo sheria inataka kuyazuia.
Profesa Kikula alisema kwa waombaji wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini baada ya kupata leseni na kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji wanatakiwa kuwasilisha Mpango wa Uhifadhi wa Mazingira.
Alisema na kusisitiza kuwa wawekezaji ambao watataka kuweka taarifa kwa lugha siyo Kiswahili au Kiingereza watakosa sifa za kupewa leseni na katika kuepuka kudanganywa, nyaraka zote zinazotakiwa inabidi ziidhinishwe na mamlaka zinazohusika na kuziwasilisha kwa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini zikiwa kamaili na kupata Baraka zake ikiwa zitafuzu.
Kesi ya Barrick Gold
Wachunguzi wa mambo wamefurahishwa na kasi ya utendaji na umahiri wa Tume kwa kuweka Sheria mbele lakini wanawasiwasi juu ya hisia na tamati ya Kampuni ya Barick Gold ambayo kwa kitendo cha kunyang’anywa Kabanga Nickel inaonekana kutakuwa na mushikeli na kwa vile kuna mtima nyongo inaonekana hataiacha nchi salama ila baada ya kulipa fidia haswa ikizingatiwa kuwa mkataba wake ulikuwa unaisha mwaka kesho, 2019.
Kwa kitendo hicho Tume imenunua kesi na kutokana na ukorofi wao tutalazimishwa kulipa fidia ya kuvunja mkataba wakitushitaki kwenye Mabaraza ya Kimataifa ya Udhamini (MIGA) na lile la Usuluhishi (IAA).
Wasiwasi huo unakuja kutokana na Barrick alikwisha kuwahi kusema kuwa wameshatumia kiasi cha zaidi ya Dola Milioni 250 katika kufanya matayarisho ya awali ili waweze kuuza mradi
Matatizo ya Barrick yamepanda baada ya serikali kurejesha madini yenye faida na hivyo Moto mkubwa wa madini wa Canada umewashwa zaidi ya dola milioni 250 yaani zaidi ya shilingi bilioni 560/- kwa zaidi ya miaka 10 katika kazi ya uchunguzi kwenye mradi wa Kabanga nickel kwa kushirikiana na Glencore .
Kampuni ya Barrick Gold, mchimbaji wa dhahabu mkubwa zaidi duniani, itaonekana kuwa ameteseka zaidi nchini Tanzania baada ya Tume ya Madini kufuta leseni yake ya uhifadhi (retention) kwa mradi tajiri wa nickel katika Mkoa wa Kagera, ambao umetokana na mwekezaji wa madini wa London, Glencore Plc.
Wadadisi waona Prof Idris Kikula, Mwenyekiti wa Tume ya Madini amekwenda haraka kutekeleza kanuni za madini ngumu zilizopitishwa na serikali mwezi Januari mwaka huu.
Leseni ya mradi wa nickel katika Wilaya ya Ngara kuanzia mwaka 2009 ilikuwa miongoni mwa Leseni 11 za uhifadhi zilizofutwa na Tume ya Madini katika mkutano wake wa kwanza wa chini ya Sheria ya Uchimbaji wa Madini ya 2017, iliyoidhinishwa Januari.
Barrick Gold Corp na Glencore Plc ambao wana mradi wa ubia wa 50:50, wameripotiwa wamewekeza zaidi ya Dola milioni 250 na leseni ilikuwa inaisha Mei 2019.
Leseni ya uhifadhi inapewa kwa wamiliki wa leseni ya kufuatilia baada ya kutambua amana ya madini ndani ya eneo ambalo linaweza kuwa na umuhimu wa biashara lakini haliwezi kuendelezwa kwa sababu ya vikwazo vya kiufundi, hali mbaya ya soko au mambo mengine ya kiuchumi ambayo inaweza kuwa ya tabia ya muda mfupi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya madini nchini Tanzania ushahidi upo unaonesha Barrick na Glencore wamekuwa wakitafuta wanunuzi wa mradi wa Kabanga tangu mwaka 2015 baada ya bei za chini za nickel duniani kupungua.
Mradi wa Eneo la utajiri wa madini linafunika eneo la zaidi ya kilomita za mraba 200, ambalo inakadiriwa kuwa na rasilimali inayofikia tani milioni 36.3, ikilinganishwa nickel 2.8%.
Kujikaanga kwa mafuta yetu
Leseni ya ‘Retention’ ni mbinu ya makampuni makubwa ya uchimbaji madini kuweza kukopa kutoka mabenki kwa kutumia maeneo hayo kama dhamana kwani yakifanyiwa utafiti wa upatikanji mali (reclaim profit) ***huchukuliwa na mabenki kama kinga tosha na hivyo hukopeshwa fedha wakati huohuo wanadai kwa serikali ya Tanzania wamewekeza kumbe walichofanya ni kufanya nchi hii kujikaanga kwa mafuta yake yenyewe. Madai ya PSA kwa serikali sio sahihi kwani hawakuwekeza kitu bali walitumia mali za serikali hiyohiyo kupata mtaji na ndio maana inaitwa ‘ kujikaanga kwa mafuta yako mwenyewe’.
Isitoshe leseni ya ‘retention’ ni kuhodhi eneo la madini na mara nyingi bila malipo au kwa malipo kiduchu na hivyo kufifisha ushindani kwani watafutaji wengine wa madini hawapati nafasi ya kuendeleza maeneo hayo na kama itapatikana ni kwa mashariti magumu na ya bei kubwa sana. Uhakika wa kuendelezwa ni finyu.
Tangazo la Taarifa
Tangazo la Tume ya Madini NA Prof Kikula lilisomeka kama; “Tungependa kuwajulisha wamiliki wote wa leseni za uhifadhi kuwa leseni zimefutwa, ”
Leseni nyingine za uhifadhi zilizofutwa na tume ya uchimbaji madini zililenga vitu vingine vya nickel, dhahabu, fedha, shaba na makampuni ya udhaifu duniani.
Rais Magufuli alituma mawimbi mshtuko kupitia jumuiya ya madini na mfululizo wa matendo tangu uchaguzi wake mwishoni mwa mwaka 2015, ambayo anasema ni lengo la serikali yake kusambaza haki ya mapato kutokana na utajiri wa maliasili kwa Watanzania.
Mnamo Julai mwaka jana, alisimamisha utoaji wa leseni zote mpya za madini kabla ya kuunda Tume mpya ya madini.
Sheria mpya
Sheria mpya za madini zilipitishwa mnamo Januari mwaka jana inasema kuwa “leseni zote za uhifadhi zilizotolewa kabla ya tarehe ya kuchapishwa kwa kanuni hizi (madini) zimefutwa na zitaacha kuwa na athari za kisheria.”
“Kwa sababu ya kufuta leseni ya uhifadhi …tamati ya haki juu ya maeneo yote yaliyomo ya leseni ya kuhifadhiwa ni hapa na bila uhakikisho zaidi unaorejeshwa kwa serikali.”
Barrick Gold Corp ya Kanada, mtengenezaji wa dhahabu mkubwa zaidi wa dunia, pia ni mbia mkubwa wa Acacia Mining Plc iliyoorodheshwa London, ambayo imehusishwa na mgogoro wa kodi unaoendelea na Serikali ya Tanzania tangu mwaka jana juu ya mauzo ya madini katika migodi yake mitatu nchini ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi.
Glencore ni kampuni ya Uswisi ya udalali wa madini, inamiliki na hufanya kazi za madini ya nickel, zinc, shaba na makaa ya mawe kote ulimwenguni.
Tume ya Madini imepewa madaraka makubwa sana ya kushughulikia masuala ya madini kwa kuzuia ulaghai wa madini na kuepuka kodi kwa makampuni ya madini na ina mamlaka ya kusimamisha na kukomesha leseni ya utafutaji na matumizi ya vibali.