31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Tuenzi Kiswahili chetu kwa kuzingatia ufasaha

Na Wardat Lupenza

LEO Julai 7, 2022 kwa mara ya kwanza Dunia inaadhimisha Siku ya Kiswahili duniani.
Maadhimisho haya yamefanyika nchi mbalimbali ikiwamo Ufaransa ambapo Msanii Mlisho Mpoto amechaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye maadhimisho hayo.

Ndugu Mhariri pamoja na Dunia kuanza kuitambua lugha yetu hii adhimu ni wajibu wetu kama Watanzania ambao ndiyo tunasifika kama kitovu cha lugha hii adhimu kukienzi na kukitunza Kiswahili.

Kwani kwa kufan ya hivyo itakuwa ni moja ya njia nzuri ya kufanikisha lugha yetu kuzungumza kwenye mataifa mbalimbali ikiwamo kufundishwa kama ambavyo tunaona kwenye mataifa mbalimbali ikiwamo Uganda, Afrika Kusini, Ethiopia na kwingine ambako lugha hii pendwa imeanzwa kufundishwa.

Hivyo, katika kuyafanikisha hayo tunapaswa kwanza kama Watanzania wenyewe tunajitahidi kuzungumza lugha yetu kwa ufasaha.

Hivyo kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo hata wasanii wetu wa fani tofautitofauti wajitahidi kuhakikisha kuwa wanatumia maeneno ya kiswahili kwa ufasaha.

Kwani kazi zao zinasikilizwa na kutazamwa na watu wengi wakiwamo wa ndani na nje ya nchi achilia mbali watoto, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa wanatumia lugha fasaha.

Ndugu Mhariri nahitimisha kwa kuwapongeza Watanzania wote na wote wanaopigana katika kuhakikisha kuwa lugha yetu ya kiswahili inafika mbali ikiwamo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO).

Mwandishi wa Maoni haya ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Tawi la Dar es Salaam(TUDARco).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles