26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

TTCL YATAKIWA KUDHIBITI UHALIFU WA KIMTANDAO

Na AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM


MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta, ameitaka kampuni ya simu za mkononi  TTCL  kuweka utaratibu  thabiti ambao utaepusha vitendo vya uhalifu wa kifedha wa mitandao hasa katika huduma za TTCL Pesa.

Akizungumza juzi wakati wa ufunguzi wa kituo cha huduma kwa wateja kilichopo katika maduka ya Mlimani City, alisema kampuni hiyo inapaswa kuhakikisha inatoa huduma salama za kifedha ili iweze kuwa mfano wa kuigwa na kampuni nyingine za simu nchini.

“Tunapenda TTCL iwe mfano wa kuigwa kwa huduma salama za kifedha,    wekeni utaratibu thabiti wa kuepukana na vitendo vya kihalifu katika huduma  hii,” alisema Meya Sitta.

Alisema TTCL inapaswa kuwa  na utaratibu wa kutoa suluhisho kwa wateja wake  haraka pindi kunapotokea makosa mbalimbali katika huduma za kifedha.

Mbali na hilo, Meya Sitta pia aliitaka kampuni hiyo kumaliza mazungumzo  haraka na kampuni nyingine za mawasiliano, ili waweze kusaini makubaliano ambayo yatafanya watumiaji wa TTCL kuweza kupata huduma za kifedha kupitia mitandao mingine.

Kwa upande wa Ofisa Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba, alisema uzinduzi wa kituo hicho ni mwendelezo wa  jitihada za kuleta mageuzi katika kampuni hiyo na kufuta utamaduni wa zamani wa kutoa huduma kwa mazoea.

Alisema katika duka hilo  huduma mbalimbali zitatolewa ikiwamo Mtendaji malipo ya bili za simu kwa wateja wa malipo ya baada  ya mauzo ya vocha kwa ajili ya muda wa maongezi na intaneti, mauzo ya simu za aina mbalimbali na vifaa kama  modemu pamoja na kutoa huduma za kifedha za TTCL PESA, ambapo wateja watapata fursa ya kutuma  na kupokea fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles