28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KAGAME AWATAKA VIJANA WAACHE FIKRA TEGEMEZI

Na ARODIA PETER, RWANDA


VIJANA Afrika wameshauriwa kuacha utegemezi wa fikra, badala yake watumie ujuzi na fursa zilizopo kwenye nchi zao kupata maendeleo.

Ushauri huo ulitolewa jana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, wakati akihutubia mkutano wa vijana kutoka vyuo vikuu, taasisi mbalimbali za vijana wajasiriamali waishio ndani na nje ya Rwanda.

Mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka nchini hapa, ukijulikana kama YouthConekt, ulifanyika juzi kwa mara ya sita tangu kuanzishwa mwaka 2012 kwa lengo la kuwakusanya vijana kujadili mambo mbalimbali.

Rais Kagame ambaye alikuwa mgeni rasmi na kutoa ushauri mbalimbali, aliwataka vijana kukaa chini na kutafuta suluhu ya matatizo yao kwa kuunganisha fikra na ujuzi kutoka kwa wengine bila kujali ni wa ndani au nje ya nchi zao.

“Huwezi kusuluhisha matatizo peke yako, amini kuna changamoto na vipingamizi, lakini usibaki kulalamika, usikae chini, simama tafuta majawabu kwa kuangalia wengine wanafanya nini, chukua kilicho chema ambacho kinakufaa.

 

“Aidha vijana bila uzalishaji ni kazi bure, usifikirie kupata kazi kwa sababu wewe ni kijana, upate kazi kwa sababu unao ujuzi wa ziada wa kazi unayoiomba.

“Mathalani, wewe ni daktari sawa, je, unakwenda kufanya kazi na chupa ya kilevi mfukoni na hivyo kusahau baadhi ya vifaa kwenye miili ya wagonjwa?” alisema Kagame.

Aidha katika mkutano huo, Kagame aliwataka vijana wa Rwanda kutatua matatizo ya nchi yao na kusahau vita na mapigano yaliyosababisha mauaji ya kimbari mwaka 1994.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles