Kinshasa, Congo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inajiandaa kumwapisha Felix Tshisekedi, kuwa rais mpya wa taifa hilo.
Sherehe za kuapishwa zinatarajiwa kufanyika Alhamisi, wiki hii na zitashuhudiwa Tshisekedi, akiapishwa kuwa rais akichukua mikoba ya Joseph Kabila, aliyeitawala Congo, tangu mwaka 2001.
Awali sherehe hizo zilikuwa zifanyike leo Jumanne, lakini Msemaji wa Muungano wa Upinzani (CACH) ambao ulimuunga mkono Tshisekedi, alisema uwezekano wa kuapishwa ni Alhamisi.
Mahakama ya katiba ilitupilia mbali madai ya mgombea aliyeshika nafasi ya pili Martin Fayulu, na kumthibitisha Tshisekedi, kuwa rais mteule wa Congo.
Tanzania, Burundi na Kenya ni miongoni mwa Mataifa kadhaa ya Afrika yaliyompongeza Tshisekedi, Â ikiwa ni pamoja na Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC.