New York, Marekani
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza mipango ya kuzindua mtandao mpya wa kijamii, uitwao TRUTH Social.
Amesema jukwaa hilo “litakabiliana na jeuri ya kampuni kubwa za teknolojia “, akizishutumu kwa kunyamazisha sauti za wapinzani huko Marekani.
Kampuni ya Trump Media & Technology Group (TMTG), ambayo yeye ni mwenyekiti wake, pia inakusudia kuzindua huduma ya usajili wa mahitaji ya video.
Trump alipigwa maarufuku katika mitandao ya kijamii au kufungiwa na mitandao kama ya Twitter na Facebook baada ya kundi la wafuasi wake kuvamia Bunge la Marekani Januari mwaka huu.
Yeye na washauri wake tangu wakati huo walidokeza kuwa wanapanga kuunda mtandao hasimu wa kijamii.
Toleo la mapema la biashara yake ya hivi karibuni, TRUTH Social, itakuwa wazi kwa wageni waalikwa mwezi ujao, na kutakuwa na “uzinduzi wa kitaifa” ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya 2022, kulingana na taarifa ya TMTG.
“Tunaishi katika ulimwengu ambao Taliban ina uwepo mkubwa kwenye Twitter, lakini Rais wako mpendwa wa Marekani amenyamazishwa,” aliandika Bw Trump.
Mapema mwaka huu, alizindua Kutoka kwa Dawati la Donald J Trump, ambayo mara nyingi ilikuwa ikiitwa blogu.