27 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yaja na mpya, Galaxy yatua kimya kimya

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kuelekea mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, klabu ya Simba imekuja na kauli mbiu mpya  inayosema  ‘Its Not Over, Kazi Iendelee’.

Mchezo huo unatarajia kupigwa Jumapili Oktoba 24 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Wekundu wa Msimbazi hao, wikiendi iliyopita wametoka kushinda ugenini  nchini Botswana, hivyo kutanguliza mguu mmoja kuelekea  hatua ya makundi.

Kocha Mkuu Didier Gomes

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 21 kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kaimu Msemaji wa klabu hiyo, Ally Shatry ‘Chico’ amesema  maandalizi kwa asilimia 80 yamekamilika na wageni wao wamewasili nchini tangu jana kimya kimya.

Chiko amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo kwa sababu wanafahamu wapinzani wao wamekuja kwa nia ya kupindua meza.

“Kama kawaida yetu kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa tunakuwa na ‘slogan’ yetu na safari hii ni ‘It Is Not Over, Kazi Iendelee’. Hii ina maana kuwa tumepata ushindi ugenini lakini kuna dakika 90 nyingine Jumapili ambazo tunahitaji kupata ushindi, kazi bado inaendelea,” amesema Chico.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles