27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Trump: Katiba haitoi haki ya uraia kwa kuzaliwa

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump amesema Katiba ya Marekani haitoi haki ya uraia kwa kila anayezaliwa hapa na kwamba ataendeleza shinikizo kukomesha utaratibu huo.

Aliandika katika ukurasa wake wa Twitter mapema wiki hii kuwa kile kiitwacho haki ya uraia wa kuzaliwa, ambacho kinaigahrimu Marekani mabilioni ya dola na kinawanyima haki raia wa Marekani, kitakomeshwa kwa njia moja au nyingine.

Aliongeza kuwa suala hilo halikuzingatiwa katika marekebisho ya 14 ya katiba kwa sababu ya kuwekewa masharti, na kumalizia kwamba wataalamu wengi wa sheria wanakubaliana na hilo.

Kipengele hicho cha 14 kilichoongezwa baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini hapa kinatoa uraia kwa yeyote aliyezaliwa katika ardhi ya Marekani, na kilinuia kutoa ulinzi wa kikatiba kwa watumwa wa zamani.

Lakini wanasiasa wa Republican akiwamo Trump, wanasema kipengele hicho kinaweka mazingira kwa watu kuingia nchini humo kinyume cha sheria na kuzaa watoto.

Lakini wakili ambaye ni mume wa mmoja wa washauri wa juu wa Trump, Kellyanne Conway, aliandika maoni katika gazeti moja kuwa hatua kama hiyo ya kukomesha haki ya uraia wa kuzaliwa itakuwa inakiuka katiba.

Awali Rais Trump alisema atatoa amri ya kirais kufuta kipengele kinachowapa haki ya kuwa raia watoto wa wageni na wahamiaji wasioruhusiwa.

Msemaji wa Ikulu ya White House, Sarah Sanders alisema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Fox News kwamba kuna zaidi ya fumbo moja kuhusu uhamiaji.

“Kuna wataalamu kadhaa wa sheria wanaodhani kwamba kuna mambo mengi huko chini, lakini suala kubwa hapa tunalopaswa kulitazama ni sababu ya kuwa katika msimamo huu kwanza,” alisema Sanders.

Alisema sababu ya hayo ni kushindwa kwa Wana-democrat bungeni kusaidia kurekebisha mfumo wa uhamiaji uliovunjika.

“Rais anaangalia njia zote, na atafanya uamuzi hatimaye kuhusu njia bora ya kuhakikisha usalama wa mipaka yetu na kusimamia sheria na utaratibu nchini mwetu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles