26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP ATANGAZA KUBADILI MTAZAMO KUHUSU SYRIA

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS Donald Trump amesema mashambulizi ya sumu nchini Syria yamebadili mtazamo wake kuhusu utawala wa Rais Bashir al Assad.

Kabla na baada ya kuingia madarakani, Rais Trump aliahidi kuimarisha ushirikiano na Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais al-Assad.

Trump alikuwa akisema jitihada za Marekani nchini Syria zitalenga zaidi kupambana na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu (IS).

Lakini hilo limebadilika baada ya kusambaa kwa video zinazoonyesha watoto wa Syria wakihangaika kupumua, wakitokwa na mapovu mdomoni huku wakionekana kuwa na maumivu makali.

Trump alisema shambulio hilo halivumiliki na limevuka mipaka.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, ameonya Marekani inaweza kuchukua hatua peke yake.

“Umoja wa Mataifa unaposhindwa kutimiza jukumu lake la kuchukua hatua, inabidi sisi wenyewe tuingilie kati,” alisema Haley.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson, alisisitiza kuitaka Urusi kufikiria upya ushirikiano wake na Serikali ya Assad.

Serikali ya Syria hata hivyo imekana kuhusika na shambulio hilo la gesi yenye sumu, ikisema ni propaganda za wapinzani wake kuwachafua na kusisitiza lilifanywa na magaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles