27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP APEWA ONYO LA KWANZA

trump_finger-jpg-crop-promo-xlarge2

NEW YORK, MAREKENI

HAIKUTARAJIWA kutokea jambo hili, lakini hiyo ndiyo hali halisi iliyopo kati ya Rais Mteule, Donald Trump na wakuu wa masuala ya usalama nchini humo. Inadaiwa kuwa, wakuu wa usalama hawafurahishwi na mwenendo wa Trump, hali ambayo imelazimika kutoa onyo kwa rais huyo mteule.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la ParsToday, Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la CIA, John O. Brennan, amemuonya Donald Trump, kutokana na msimamo wake kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 yanayojulikana kwa jina la JCPOA na kusisitiza kuwa, haitakuwa busara hata kidogo kufutwa makubaliano.

Mkurugenzi huyo ameonya kufutwa makubaliano hayo kutazipelekea nchi nyingine duniani zipate nguvu za kuendelea na miradi yao ya nyuklia.

“Ninavyoamini mimi kama makubaliano hayo yatafutwa, kutazuka balaa kubwa na hatua hiyo itakuwa haijawahi kuchukuliwa mfano wake katika historia nzima ya Marekani,” alisema Brennan.

Onyo la kiongozi wa ngazi za juu wa masuala ya usalama nchini humo kuhusu hatari ya moja ya ahadi kuu za Donald Trump alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi, yaani kufuta makubaliano ya nyuklia, kwa hakika linadhihirisha wasiwasi ilio nao serikali ya hivi sasa ya Marekani kuhusu utendaji wa serikali ijayo ya nchi hiyo.

Ni wazi kuwa, iwapo Trump ataamua kufuta au kufanyia marekebisho makubaliaho ya JCPOA, ambayo yamefikiwa baada ya juhudi kubwa za kimataifa, kutaipotezea heshima ya Marekani.

Makubaliano hayo si makubaliano ya pande mbili za Marekani na Iran, bali Marekani ni sehemu tu ya nchi sita kubwa duniani zilizofikia makubaliano hayo na Iran.

Nchi nyingine tatu za Ulaya waitifaki wa Marekani zilizoshiriki kikamilifu kwenye mazungumzo yaliyozaa makubaliano ya nyuklia ni Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na China.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nalo lilishiriki kikamilifu kwenye ufanikishaji wa makubaliano hayo na Julai 2015, lilipitisha azimio nambari 2231 la kupasisha utekelezaji wa makubaliano hayo.

Makubaliano hayo, yaliyopata baraka kamili za kimataifa, yalianza kutekelezwa mwaka huu na tangu wakati huo, Iran imetekeleza kikamilifu ahadi zake zote na hilo limethibitishwa na ripoti za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Kwa upande wa nchi za Ulaya pia, kutokana na matatizo yao mbalimbali ya kiuchumi, zimeonesha hamu kubwa ya kuimarisha uhusiano wao wa kiuchumi na kibiashara na Iran, hivyo nazo zimeamua kutilia mkazo uhakika kuwa Iran imechukua hatua zinazotakiwa kwa mujibu wa makubaliano. Lakini zimesisitiza hazifurahishwi na ukwamishaji wa kila namna unaowekwa na Marekani katika utekelezaji.

John O. Brennan amemwambia wazi Trump kuwa kufuta makubaliano hayo si tu kutaipotezea heshima kimataifa na kuionesha kuwa ni nchi isiyo na mwamana, lakini pia nchi nyinginezo duniani nazo zitapata nguvu kwa kuendelea na miradi yao ya nyuklia na hazitakuwa tayari kusikiliza ahadi zisizo na dhamana ya kutekelezwa.

Iran yaichokoza Marekani

Katika hatua nyingine, Mjumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge la Iran, Akbar Ranjbarzadeh, amesema wabunge wanaandaa hoja ya dharura wa kujadiliwa haraka na nje ya utaratibu wa kawaida wa kuanzisha tena mchakato wa nyuklia kwa lengo la kukabiliana na Marekani.

Ranjbarzadeh amesema hatua ya Bunge la Seneti la Marekani ya kurefusha kwa miaka 10 mingine sheria ya vikwazo dhidi ya Iran ni ukiukaji wa makubaliano ya nyuklia (JCPOA).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles