31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TRA YAWANOA WAJASIRIAMALI

download

Na JACQUILINE MRISHO – MAELEZO.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo kwa wajasiriamali kuhusu kodi   waweze kufahamu aina na madaraja ya kodi pamoja na umuhimu wa ulipaji kodi.

Mafunzo hayo yalitolewa jana na Ofisa wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, George Haule katika semina ya wanawake wajasiriamali iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) katika viwanja vya Sabasaba, Dar es Salaam.

Haule alisema katika uanzishaji wa biashara ya aina yoyote jambo la kwanza na muhimu ni kujisajili katika mamlaka hiyo na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN – Number) itakayomuwezesha mfanyabiashara au mjasiriamali kuwa na biashara halali ambayo inalipiwa kodi kulingana na mauzo au faida ya biashara husika.

”Tanzania ni nchi yetu na sisi Watanzania ndiyo tuna jukumu la kuitunza nchi hii, njia rahisi ya kuitunza nchi ni kulipa kodi stahiki  kuinua pato la taifa kwa sababu kodi ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya nchi,”alisema Haule.

Alisema Serikali ya Tanzania inatumia mfumo endelevu wa ulipaji kodi kwa maana ya kila mfanyabiashara mdogo mwenye mauzo yasiyozidi Sh 20,000,000 kulipa kodi ya mwaka kulingana na mauzo yake na mwenye mauzo yatakayozidi kiasi hicho cha fedha kulipa kodi ya mwaka kulingana na faida anayoipata katika biashara husika.

“Wafanyabiashara wadogo wamegawanyika katika makundi matano ambako wenye mauzo ya kuanzia Sh 1 hadi Sh 4,000,000 kwa mwaka hawalipi kodi yoyote, wenye mauzo kuanzia Sh  4,000,000 hadi Sh 7,500,000 wanalipa kodi ya Sh 150,000 kwa mwaka.

“Wenye mauzo kuanzia Sh 7,500,000 hadi Sh 11,050,000 wanalipa Sh 318,000 kwa mwaka, wenye mauzo kuanzia Sh 11,050,000 hadi Sh 16,000,000 wanalipa Sh 546,000 kwa mwaka na wenye mauzo kuanzia Sh 16,000,000 hadi Sh 20,000,000 wanalipa Sh 862,000,”alisema Haule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles