31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KAULI YA MWIGULU KUHUSU MAITI MTO RUVU YAZUA MASWALI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba

MAULI MUYENJWA-DAR ES SALAAM

KAULI ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kuhusu kauli yake kwamba maiti saba zilizokutwa Mto Ruvu zikielea, walikuwa ni wahamiaji haramu, imezua maswali lukuki.

Nchemba alitoa kauli hiyo jana asubuhi katika  kipindi cha ‘Tuongee Asubuhi’, kinachorushwa moja kwa moja na Kituo cha luninga cha Star Tv.

Desemba 7 mwaka huu, miili ya watu hao ilikutwa kando ya Mto Ruvu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa imewekwa ndani ya mifuko ya sandarusi na ndani yake yakiwa yamewekewa mawe ili isielee kisha mifuko hiyo kushonwa kama mzigo wa mazao na kutupwa mtoni.

Baada ya kauli hiyo ya Waziri Nchemba, watu wengi katika mitandao ya  jamii jana walihoji uhalisia wa kauli hiyo na wengine kuonyesha wasiwasi juu ya ukweli wa suala hilo.

Mmoja wa waliojadili kauli hiyo aliyejitambulisha kama raia wa kawaida, Martine Mayanja, alihoji, “kwa nini miili ile ilizikwa haraka na serikali kabla hata ya kupimwa vinasaba (DNA) na kutambulika na ndugu wa marehemu?”

“Hata kama watu wale walikuwa ni wahamiaji haramu, je, hiyo ndiyo njia ya kuwadhibiti.  Je ndiyo wanapaswa kuuawa kwa ukatili namna ile na kutupwa kwenye mto Ruvu?

“Sheria za nchi, sheria za jeshi la polisi na Idara ya Uhamiaji zinasemaje kuhusiana na wahamiaji haramu?  Na kama wale ni wahamiaji haramu nani ametoa idhini ya kuwaua na nani kawaua. Kwa nini watupwe mto huo wakiwa wamefungwa mawe ili wazame wasionekane,” aliendelea kuhoji.

Maswali mengine yalihusu miili ya maiti hizo kuonekana kujehuriwa huku mamlaka, akiwamo Nchemba, wakiwa kimya juu ya suala hilo.

Mwananchi mwingine kwenye mtandaowa  Jamii Forum, alisema:  “Kama taarifa hizo niza kweli basi anaona uwakilishi wa suala hilo kwa umma haukuangalia madhara yake kwenye uhusiano wa kimataifa na ndani pia.

“Ni vizuri msemaji (waziri) angesema kwamba uchunguzi umeshindwa kuwatambua wahusika na uchunguzi unaendelea kwa kuwa hakuna mtu ambaye alikuwa amejitokeza wazi wazi kudai kupotelewa na ndugu yake. Kauli ya waziri kwamba hao ni wahamiaji haramu bado hai -“justify” tukio hilo,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles