24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TRA, Taffa kutoa mwongozo wa ulipaji kodi

Na BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa) kutoa mwongozo kwenye baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi kwa wafanyabiashara kulipa ipasavyo.

Alisema jingine ni wafanya biashara wanaweza kubadilisha tini namba zao binafsi na kuweza kununulia vitu nje ya nchi kupitia tini namba yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Makamu wa rais wa Taffa, Waheed Saudin wakati wa wakutoa semina ya mafunzo kwa wafanyabiashara  jinsi ya kutumia tini namba na binafsi kufanya na kutumia risiti za kieletroniki wanapouza na kununua bidhaa.

“Niwajibu wetu kuona kodi zote za serikali zinalipwa ipasavyo ili kuhakikisha waliokuwa wakifanya tini namba zao binafsi kuweza kufanya kuwa za kibiashara,” alisema.

Alisema wanatoa mafunzo hayo kwa walipa kodi kwa kuwa, Ritani ya VAT imefanyiwa maboresho mbalimbali ikiwemo eneo la ujazaji na viambatanisho vyake hivyo ni vema wakatoa mafunzo hayo kwa wafanyabishara waliosajiliwa na VAT ili wajue namna ya ujazaji wa marekebesho katika Ritani kabla ha mfumo wenyewe kuanza kufanya kazi.

Kwa upande wake, Ofisa usimamizi wa kodi, George Haule alisema kuwa wameamua kufanya semina na Taffa kwa sababu wao ndio wanaojihusisha na watu wanaoingiza bidhaa katika nchi hii, hivyo wanahusika katika masuala ya kodi.

“Tumeelekezana mambo makubwa mawili jinsi ya kutuma kutuma ritani za kikodi wanapotuma tunazipata kwa wakati na kufanya shughuli zingine.

“Kusaidia TIN ambapo TRA imefanya utaratibu wa kubadilisha kuwa mfanyabiashara ana uwezo wa kutumia TIN binafsi kuagizia magari na mizigo mingine lengo ni kubana watu wasitumie kwa lengo lingine la kuagiza magari ya biashara labda iwe moja la mtu binafsi na kuweza kuzuia mapato ya serikali yasitumike ovyo.

“Kwa kupitia mfumo huo mfanyabiashara ataweza kufanya marekebisho mwenyewe ya Ritani za VAT bila ya kuandika barua kama awali ambapo huku pia maboresho makubwa yakiwa yamefanywa katika eneo la kuweka risiti za kietroniki ambazo zinakuwa hazijajazwa .

“Zamani mtu alikuwa anaweza kujaza Ritani na kuweka risiti hata kama ameiokota lakini baada ya Maboresho haya mtu hataweza kujaza Ritani katika risiti isiyokuwa ya Kwake,” alisema Haure.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles