28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

TRA: Mfumo mbovu unawanyima wamiliki wa mabasi mapato

Na Koku David, Dar es Salaam

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Edwin Mhede amesema utafiti unaonyesha Sh milioni 67 hupotea kwa siku ambapo ni sawa na Sh bilioni 24.4 kwa mwaka katika mabasi 4,500.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa kikao cha mafunzo kuhusu mfumo wa mtandao katika ukatishaji wa tiketi na kushirikisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), TRA na wamiliki wa makampuni mbalimbali ya mabasi ya usafirishaji.   

Dk. Mhede alisema kuanza kutumika kwa mfumo wa mtandao katika ukataji wa tiketi utasaidia kuondoa urasimu na upotevu wa mapato kiholela kwa serikali na wamiliki wa sekta binafsi.

“Kwa utafiti uliofanyika kwa kipindi cha miezi mitano kuanzia Julai mpaka sasa unaonyesha Sh milion 67 zinapotea kwa siku ambazo ni sawa na Sh bilion 24.4 kwa mwaka katika mabasi 4,500,” alisema Dk Mhede.

“Kwa mfumo unaotumika sasa unawafanya wamiliki wa makampuni ya mabasi kupoteza  asilimia 70 hadi 73 huku wakipata asilimia 27 mpaka 30 za mapato ambayo yalikuwa haki yao,” alisema Dk. Mhede.

Dk. Mhede alisema kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kati ya mabasi 4,500 yanayofanya masafa marefu nchi nzima na ambayo yamesajiriwa na LATRA inaonyesha Sh milioni 536 ambazo ni sawa na Sh bilioni 166 hazijulikani zinakokwenda ambazo ni haki ya wamiliki hao nje ya kodi wanazolipa.

Alisema anatamani kuona faida hiyo inayopotea ambayo ni haki ya wamiliki wanaipata ili waneemeke ikiwa ni pamoja na wao kuongeza ulipaji wa kodi sawa sawa na mapato wanayoyapata.

Ameongeza kuwa moja ya sababu ya kupotea kwa mapato ni usimamizi duni wakutokuwa na kumbukumbu za mwenendo wa biashara yako na kwamba kuanza kutumika kwa mfumo huo kutaondoa udalali unaotumika sasa baina ya wateja na watumishi wa mamlaka hiyo na kuwezesha kila mmoja kupata pesa yake halali.

“Nawapongeza LATRA kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo inalenga kuokoa mapato kwani mpaka kufika mwezi June mwaka wa fedha waliweza kukusanya takribani Sh bilioni 20.6 sawa na malengo kusudiwa,” alisema Dk. Mhede.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Gilliard Ngewe aliipongeza TRA kwa kuanzisha mfumo huo ambao utakuwa na tija kwa serikali na wamiliki kwa ujumla na kwamba LATRA ipo tayari kuutumia ikiwa ni pamoja na kuanzisha ofisi mikoa yote.

Alisema mfumo huo una faina kubwa ambazo ni zitawezesha usimamizi mzuri na umakini wa sheria za LATRA, kuimarisha usalama baina ya watumishi na wateja, kulinda maslahi ya watumiaji na abiria pamoja na kuleta maslahi ya kiuchumi katika ukusanyaji wa kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles