27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC YACHAGIZA MAFANIKIO  MIAKA 56 YA UHURU TANZANIA

 

Na Mwandishi Maalumu


TUKIWA tunatimiza miaka 56 ya uhuru kila Mtanzania anajambo la kujivunia ambapo yapo ya kiujumla na binafsi lakini tukiwa kama Taifa lenye changamoto ya kukuza uchumi wake kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 yapo mambo ambayo tumekuwa tukiayaangalia na kuyapa uzito kama moja ya vitu vya kutufikisha huko na mambo hayo kwanza ni rasilimali au utajiri tulio nao kama watanzania ambazo hujumuisha rasilimali watu, ardhi, mito, maziwa, bahari, madini, mbuga za wa wanyama, mazao na gesi asilia kwa uchache tu.

Tunapotimiza miaka 56 ya Uhuru wetu tuangalie sekta ya nishati na hapa tutaangazia shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia, mafanikio, mchango wake na mipango ya baadae. Serikali imekabidhi shughuli hizi kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ili kuzisimamia na kuendesha kwa maslahi mapana ya Taifa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba yeye anaiongela Miaka 56 ya Uhuru kama ni kipindi cha mafanikio makubwa yaliyoletwa na utawala katika awamu zote tano za Serikali.

“Sisi kama TPDC kwanza tunaunga mkono kwa dhati kabisa kwa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli, Serikali yake na Watanzania wote katika kusheherekea Miaka 56 ya Uhuru wa Nchi yetu na pia tunazipongeza awamu zote za Uongozi katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Tanzania na kwa dhati kabisa Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere katika juhudi zake na mafanikio katika vita dhidi ya Ukoloni,” alifafanua Kaimu Mkurugenzi.

Mhandisi Msomba anaeleza kuwa, “Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ni moja ya zao la Uhuru wa Tanzania uliopatikana mwaka 1961 na lilianzishwa kuptita Tangazo la Serikali namba 140 la tarehe 30 Mei, 1969 kupitia Sheria ya Mashirika ya Umma namba 17 ya mwaka 1969 na kuanza rasmi kufanya kazi mwaka 1973 na hivyo linamilikiwa na Serikali na hisa zake zote zinashikiliwa na Msajili wa Hazina.”

Mhandisi Msomba anaeleza kuwa kwa TPDC katika kuadhimisha Miaka 56 ya Uhuru ni kwake kuchagiza ukuaji wa kasi wa uchumi wa Tanzania haswa kwa kupitia ukuaji wa sekta ya viwanda kwa kuhakikisha uwepo wa gesi asilia ya kutosha na kuisambaza kwenye viwanda mbalimbali.

“Toka awamu ya kwanza ya Serikali iliyoongozwa na Baba wa Taifa shauku kuu ilikuwa kujenga Tanzania ya viwanda na yenye uchumi wa kujitegema. Mwalimu alivutiwa sana na uchumi wa viwanda na hivyo alijitahidi kuona Tanzania inakuwa Taifa huru kiuchumi kwa kuwa na viwanda vya kutosha na hivyo toka awamu ya kwanza hadi sasa tumeona juhudi za kuifanya nchi yetu kuwa ya viwanda na sisi kama TPDC tunaona fahari kuwa sehemu kubwa ya utekelezaji wa mpango huo wa kuijenga Tanzania ya viwanda.”

“Ni kazi kwa wananchi kuelewa moja kwa moja mchango wa TPDC katika uchumi wa Viwanda wa Nchi yetu kwakuwa sisi ni msingi katika maana tunawezesha  TANESCO kuzalisha umeme kwa matumizi ya nchi na hivyo wananchi wataona tu umeme upo wa kutosha lakini jambo tunalojivunia sisi kama TPDC ni kuona tunachangia zaidi ya asilimia 50 ya umeme unaozalishwa kwenye gridi ya Taifa. TPDC pamoja na kusambaza gesi asilia yenye unafuu wa zaidi asilimia 30 ya gharama ya mafuta katika matumizi ya viwandani,” alieleza Mhandisi Musomba.

Ni wajibu wa TPDC katika maadhimisho haya kujikita katika utafiti zaidi wa gesi asilia na mafuta katika maeneo mbalimbali ya nchi yakiwemo Eyasi Wembere, Songo Songo West na kwenye vitalu vya 4/1B na 4/1C kupitia Idara yake ya Mkondo Wajuu ili kuweza kuongeza thamani ya vitalu hivyo na pengine kuweza kupata gesi asilia au mafuta katika siku za usoni. Lakini pia kuhakikisha gesi asilia inaendelea kusambazwa katika mitambo ya kufua umeme ya sasa na inayoendelea kujengwa pamoja na kusambaza gesi asilia kwa viwanda vilivyopo na vipya, kusambaza gesi asilia majumbani na kuongeza watumiaji wa gesi asilia kwenye magari, Mhandisi Musomba alisisitiza.

Kihistoria shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia ni kongwe kuliko uhuru wetu tunaambiwa kuwa utafiti wa mafuta na gesi asilia una zaidi ya miaka 60 nchini Tanzania.

Kaimu Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu wa TPDC Venosa Ngowi anaeleza kuwa utafiti wa mafuta ulianza kabla ya Uhuru mnamo mwaka 1952 ambapo kampuni ya Ubia kati ya British Petroleum (BP) na Shell International (SHELL) walianza utafutaji wa mafuta katika mwambao wa Afrika Mashariki pamoja na mwambao wa Tanzania.

“Kwa muktadha  huu TPDC imetenga historia ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika awamu tano yaani Awamu ya Kwanza 1950-1964, Awamu ya Pili 1969-1979, Awamu ya Tatu 1980-1991, Awamu ya Nne 1992 hadi 1999 na Awamu ya Tano mwaka 2000 hadi sasa” anabainisha Bi Ngowi.

“Mwaka 1964 AGIP ilipewa maeneo yaliyokuwa ya BP/SHELL na mwaka 1973 iliungana na AMOCO ambapo walichimba visima vitano ambavyo ni Ras Machuisi na SS1 mwaka 1974, Kisangire na Kisarawe mwaka 1976 na Kizimbani 1979 ambapo kisima cha SS1 kiligundulika kuwa na gesi asilia kiasi cha futi za ujazo bilioni 4 (4BCF) kiasi ambacho AGIP walikiona kidogo kiuchumi na hivyo waliamua kuachia eneo lote la Songo Songo,” anaeleza Venosa.

Baada kurudishiwa eneo la Songo Songo, TPDC ilifanya tathimini zaidi ya data na hifadhi ya gesi ambapo ilikusanya data za mitetemo na kuchimba visima vitatu ambavyo ni SS2,SS3 na SS4 kutokana na tathimini ya TPDC ilionekana kuwa eneo hilo lina kiasi cha gesi asilia futi za ujazo trilioni moja na si bilioni nne kama AGIP walichogundua.

“Mnamo mwaka 1982 AGIP iligundua tena gesi asilia kwa mara ya pili katika eneo la Msimbati Mkoani Mtwara na TPDC ilijikita katika ukusanyaji wa takwimu zaidi katika maeneo ya nchi kavu na majini ili kuvutia wawekezaji,” anaeleza ndugu Venosa.

Shirika lilichimba visima vitano vya kuthibitisha (appraisel wells) ambavyo ni SS5, SS6, SS7, SS8 na SS9 katika eneo la Songo Songo apmoja na visima hivyo pia kulishuhudiwa na uchimbaji wa visima vitatu vya utafutaji TanCan1 (Majini), Kimbiji East na Kimbiji Main vya nchi kavu pamoja na ukusanyaji wa takwimu za graviti katika eneo la Rukwa.

Katika kipindi cha awamu ya nne TPDC kwa kushirikiana na kampuni ya WesternGeco walikusanya takwimu za mitetemo za 2D katika kina kirefu cha bahari ili kuweza kujiridhisha na utajiri wa bahari kuu katika uhifadhi wa gesi asilia na mafuta kwa pamoja walifanya zoezi hilo katika awamu mbili yaani mwaka 1999 ambapo jumla eneo la mraba la 6700KM lilifanyiwa utafiti na kupata takwimu za mitetemo na amwamu ya pili ni mwaka 2000 ambapo jumla ya eneo la mraba la 4735Km ilifanyiwa utafiti zoezi hili ndilo limechagiza utafutaji wa kina kirefu cha habari unaoendelea hadi sasa pamoja na ugunduzi mkubwa wa gesi asilia.

Katika kipindi hiki cha awamu ya nne na awamu ya tano hadi kufikia mwaka 2012 maeneo makubwa ya bahari na nchi kavu yalikuwa yamefanyiwa utafiti na kupatikana kwa takwimu za mitetemo za 2D na 3D ambapo jumla ya kilomita za mraba 25,875 za nchi kavu zilikuwa zimefanyiwa utafiti na kupatikana kwa takwimu za 2D. Maeneo ya kina kifupi na kirefu ya bahari yenye ukubwa wa kilomita za mraba 72,281 yalishafanyiwa utafiti na maeneo ya kina kirefu zaidi (ultra-deep) yenye ukubwa wa kilomita za mraba 10,151 kutokana na utafiti wa maeneo hayo jumla ya twakwimu za 2D zilizopatikana ni 108,307 kilomita za mraba na 15,644 kilomita za mraba za 3D.

Aidha kwa mujibu wa mawasilisho ya TPDC kwenye utoaji elimu inaonekana kuwa katika awamu hii Serikali iliboresha zaidi Mkataba wa Ugawanaji wa Mapato (Production Sharing Agreement) na kuongeza juhudi katika kunadi maeneo na kushawishi makampuni kuchukua maeneo hayo nchini na mafanikio yake yalikuwa mazuri kwakuwa makampuni yapatayo 17 yaliingia nchini na kusaini mikataba ya utafiti ipatayo 25 hadi kufikia 2014.

Zoezi la kunadi vitalu lilihusisha duru zipatazo nne ambapo ya kwanza ilifanyika Houston nchini Marekani mwaka 2000 na zabuni moja toka kwa Petrobras ilipokelewa na mnamo 2004 kampuni hiyo iliingia mkataba wa utafutaji wa kitalu namba tano, Duru  ya pili ilifanyika mwaka 2001 AAPG, Denver, Colorado nchini Marekani na kufungwa mwaka 2002 ambapo kampuni ya SHELL ilishinda vitalu namba 9 hadi 12.

Duru ya Tatu ilizunduliwa nchini Uingereza mwaka 2004 ambapo vitalu namba 1,2,3,4,6,7 na 8 ambavyo havikupata wateja katika duru zilizotangulia vilinadiwa na matokeo yake yalikuwa kampuni ya Ophir ilishinda kitalu namba1, Statoil namba 2, Petrobras namba 6 ambapo hadi kufikia 2007 mikataba na makampuni haya ilikuwa imeshasainiwa.

Kwa mara ya kwanza mnada katika Duru ya nne uliendeshwa hapa nchini Tanzania jijini Dar es Salaam mwaka 2013 ambapo vitalu saba vya kina kirefu vilinadiwa 1B, 1C, 2A, 3A, 4A, 4B, 5A NA 5b hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2014 ambapo tenda ilifungwa, tenda tano zilipatikana za CNOOC kitalu nama4/3A, RAKGAS alipata Ziwa Tanganyika Kaskazini, Statoil na ExxonMobil kitalu nama 4/3A, Mubadla kitalu namba 4/2A na gazProm kitalu namba4/3B

Jitihada zote hizi za Shirika toka kuundwa kwake mwaka 1969 zimeweza kuzaa matunda makubwa hadi sasa haswa tukishuhudia ugunduzi mkubwa wa gesi asilia ambapo kiasi cha futi za ujazo wa futi za ujazo trilioni 57.25 ambapo kiasi cha futi za ujazo trilioni 10 pekee ni zimegundulika nchi kavu na kiasi kilichobaki cha futi za ujazo trilioni 47.25 kimegundulika baharini.

Ugunduzi wa kwanza ulifanyika mwaka 1974 katika Kisiwa cha Songo Songo Mkoani Lindi kiasi cha futi za ujazo bilioni nne kabla ya TPDC kufanya tafiti zaidi ambazo zilidhihirisha kiasi kilichopo ni futi za ujazo trilioni moja na ugunduzi wa pili ulikuwa wa Mnazi Bay Mtwara mnamo mwaka 1982.

Kwa ujumla wake toka shughuli za utafiti zianze Nchini Tanzania jumla ya visima vilivyochimbwa ni 95 na ni asilimia hamsini tu ya visima hivi ndivyo vimeweza kugundulika gesi asilia ambapo ugunduzi mkubwa ulifanywa katika vitalu vya baharini.

Hadi sasa maeneo ambayo yamegundulika kuwa na gesi asilia nchini ni Songo Songo, Mnazi Bay, Ntorya, Mkuranga, Ruvu na katika vitalu vya Bahari Kuu.

Ujenzi wa bomba la gesi

Katika miradi ya mafanikio ya kujivunia kwa TPDC ni ule wa ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam wenye thamani ya Dola Bilioni Mbili na umbali wa kilomita .. na kuiwezesha Dar yenye Soko la gesi hiyo kufikika kirahisi na kutamba kushiriki au kuwa na mapinduzi ya Uchumi wa Viwanda. Tpdc NI MSINGI WA upatikanaji wa Nishati ya Uhakika kutokana na gesi na karibu itashugulikia upatikanaji uwekezaji wa mtambo wa LNG kuchakata gesi kwa ajili ya mauzo ya nje. Hapo tukifikia tutambua umuhimu wa TPDC, gesi asilia na uhuru wetu wa kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles