26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC kulinda mazingira kwa kuhamasisha matumizi ya gesi asilia

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema litahakikisha linasambaza gesi asilia kwa wananchi pamoja na kutoa elimu sahihi ya mazingira ili kunusuru wimbi la ukataji miti kwa ajili ya shughuli za kibinaadamu katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamebainishwa Februari 11, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk. James Mataragio, ambapo alisema kuwa wanajua juu ya kuwapo kwa uchafuzi wa mazingira unaotokana na ongezeko la ukataji miti hivyo ndiyo maana wamekuja na mkakati wa usambazaji gesi asilia.

“Tunajua kuwa kumekuwa na ukataji miti mkubwa unaoendelea nchini na ndiyo sababu TPDC tukaja na mkakati wa kusambaza nishati ya gesi asilia kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwamo kupikia na kuendeshea viwanda.

“Hivyo tunaendelea kutoa elimu sahihi juu ya matumizi ya gesi ikiwamo kuwaeleza umuhimu wa kutumia nishati hiyo ambayo kwa kiwango kikubwa ni rafiki kwa mazingira yetu.

“Lakini mbali na kupikia na kutumika viwandani pia tunaendelea kuhamasisha weye magari kutumia gesi asili badala ya mafuta yanayochafua pia mazingira,” amesema Dk. Mataragio.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia kuwaunganishia wateja wa viwanda maeneo ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani (Picha na Maktaba).

Kwa mujibu wa Dk. Mataragio, wananchi wengi wameendelea kuunganishwa kwenye matumizi ya gesia asilia kwenye Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara na kwamba kinachoendelea kwa sasa ni kuendelea kusambaza huduma hiyo kuwa jirani zaidi na wananchi.

“Kutokana na ongezeko hilo, kituo cha sasa cha (CNG) kilichopo Ubungo, kinashindwa kuhimili matakwa ya matumizi hivyo shirika linaendelea na ujenzi wa vituo vingine kwenye eneo la Ubungo ilipokuwa stendi ya mabasi zamani, kinachotarajiwa kuzinduliwa Machi Mosi, mwaka huu.

“Kituo hicho, kitatumika kujazia gesi katika magari yakiwamo yale yaendayo haraka pamoja na kupeleka gesi maeneo ambayo miundombinu ya mabomba ya gesi bado haijafika, yakiwemo maeneo ya viwanda Kigamboni na Kibaha pamoja na maeneo ya Feri na Muhimbili, hivyo tunaendelea kuongeza mindombinu,” amesema Dk. Mataragio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles