24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

TPB yatoa msaada kwa Jeshi la Polisi

camillius-wamburaNa MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

BENKI ya Posta Tanzania (TPB), imetoa msaada wa kompyuta mbili na samani za ofisi, vyote vina thamani ya Sh milioni nane kwa Jeshi la Polisi.

Msaada huo ulikabidhiwa jana kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Camillius Wambura na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Jema Msuya.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Msuya alilipongeza Jeshi hilo kwa kazi nzuri ambayo limekuwa  linaifanya ya kulinda usamala wa raia na mali zao.

“Lakini pia mmekuwa mkilinda usalama katika sekta mbalimbali hususan za fedha, tunaamini vifaa hivi vitakwenda kusaidia huduma mbalimbali mnazozitoa kwa raia pamoja na kuongeza ufanisi wa kazi nchini,” alisema Msuya.

Aidha, Msuya alitumia nafasi hiyo kuzikumbusha taasisi nyingine kujitokeza kusaidia Jeshi la Polisi katika kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili hususan  vitendea kazi.

Kwa upande wake, Wambura alisema amepokea kwa furaha msaada huo kutoka kwa Benki ya Posta kwani utawasaidia sana katika shughuli zao za kila siku.

“Tunaishukuru sana Benki ya Posta Tanzania kwa msaada huu na tunaamini utatusaidia sana katika shughuli zetu za kila siku, hasa katika suala zima la kuweka kumbukumbu ili kuboresha ulinzi wa raia na mali zao,” alisema.

Aidha, alisema msaada huo ni mfano tosha kuwa TPB inashirikiana vizuri na taasisi za ulinzi na usalama kuboresha ustawi wa jamii nzima kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles