24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

TP Mazembe yaimwagia siri Stars

Mois_Katumba_TP_Mazembe_Esaja_Yes_AfricanNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

MMILIKI wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi, ameipa siri ya ushindi timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, itakayosaidia kuwaua vinara wa soka barani Afrika, Algeria, ili kukata tiketi ya kusonga mbele kwenye michuano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Jumamosi iliyopita TP Mazembe ilikutana na timu ya USM Alger ya Algeria katika mchezo wa awali wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuichapa mabao 2-1 ugenini na kujitengenezea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa watakaporudiana.

Habari za uhakika ambazo zimelifikia MTANZANIA jana kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Kamati ya Ushindi ya Stars, zimedai kuwa kigogo huyo alishauri timu hiyo kutumia mbinu walizotumia za kukwepa hujuma ambazo ziliwapa ushindi ugenini dhidi ya wapinzania wao.

Amewataka viongozi wa Stars kuhakikisha hawaendi moja kwa moja nchini Algeria kwenye mchezo wa marudiano, badala yake watafute kituo cha karibu ambacho watafikia ili wapate urahisi wa kuunganisha na kutua kwenye ardhi yao muda mfupi kabla ya mechi.

“Wenzetu wanadai walilazimika kuweka kituo katika mji wa Marrakech, nchini Morocco, ambapo ni umbali wa kilomita 1,765 kufika Algeria ambapo unaweza kutumia muda wa saa moja kufika nchini humo kwa usafiri wa ndege kutokana na ukaribu uliopo,” alisema kiongozi huyo.

Alisema wameshauriwa kutumia njia hiyo kama mbinu ya kusaka ushindi, ambayo itawasaidia kuepuka vitendo visivyo vya kiungwana wanavyoweza kufanyiwa wakiwa nchini humo, ambapo amedai kuwa wameupokea ushauri huo na wataufanyia kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles