33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi waimarisha ulinzi kuapishwa Dk. Magufuli

magulVERONICA ROMWALD NA GODFREY MBANILE (GPC), DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi limesema limeimarisha ulinzi kesho wakati wa kuapishwa Rais mteule wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli.

Sherehe za kuapishwa Dk. Mgufuli zitafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam  ambapo  viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamishna wa Oparesheni Maalumu wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja,  alisema ni marufuku kwa wananchi kushiriki katika maandamano yaliyoandaliwa bila kufuata taratibu za nchi.

“Tunawashukuru wananchi na vyombo vya habari kwa sababu  kwa pamoja tulishirikiana katika kipindi cha uchaguzi ambacho kilikuwa ni cha vuta nikuvute na tumeweza kuilinda amani yetu hadi hii leo.

“Hatimaye kesho tunatarajia kuapishwa kwa rais mteule,  Dk. Magufuli, nawasihi wote kwa pamoja tuendelee na moyo huo huo  wa kulinda amani yetu.

“Tusishiriki kabisa maandamano batili kwa sababu  yanaweza kusababisha  uvunjifu wa amani na jeshi hatutasita kuwachukulia hatua watu watakaokaidi agizo hili,” alisema.

Aliwataka wananchi na waandishi wa habari kutoa ushirikiano wakati wa kuapishwa kwa Dk. Magufuli kwa kutoa taarifa iwapo watabaini kuwapo  viashiria vya uvunjifu wa amani kama   walivyofanya katika kipindi cha kampeni na uchaguzi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa,” alisema.

Akizungumzia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yaliyotarajiwa kufanyika   jana, alisema polisi walilazimika kuyazuia kwa vile  yalikosa sifa kutokana na maombi kuwasilishwa nje ya muda unaotakiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles