25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mhandisi jela kwa rushwa

NA BEATRICE MOSSES, BABATI

MHANDISI wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Baslid Mlay, amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya Sh milioni 1.5 baada ya kupatikana na hatia ya kuomba rushwa ya Sh milioni saba.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 118 ya mwaka 2013, Mlay ambaye alishtakiwa kwa tuhuma sita, alitiwa hatiani kwa makosa matatu ambapo kila kosa alihukumiwa kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh 500,000.

Akisoma hukumu hiyo mjini Babati, Hakimu Mkazi  Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Devota Kamuzora, alisema Mlay alitenda makosa hayo Desemba 13, mwaka 2012.

Waendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Plasidya Henry na Yahaya Masakilija, wakiongozwa na Mwendesha Mashtaka Mkuu, Isdory Kyando, walidai Mlay aliomba na kupokea rushwa kutoka kwa Joseph Matiko.

Alidai siku ya tukio, Mlay aliomba kiasi hicho kwa mkandarasi wa maji  aliyetajwa kwa jina moja la Matiko, mkazi wa  Dar es Salaam ili aweke saini kwenye kibali chake cha kukamilisha kazi ya mradi wa maji wilayani humo.

Alidai kuwa Mlay aliomba fedha nyingine alizopatiwa na Matiko kwa njia ya Airtel Money na kiasi kingine aliwekewa kwenye akaunti yake ya Benki ya NMB tawi la Mbulu.

Hakimu Kamuzora alimtia hatiani kwa makosa matatu.

Kosa la kwanza  alihukumiwa   kutumikia kifungo cha miaka miwili au kulipa faini Sh 500,000.

Kosa la pili  alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh 500,000 na kosa la tatu miaka miwili jela au kiasi kama hicho. Mshtakiwa alilipa faini hiyo.

Hakimu Kamuzora aliagiza Mlay azirudishe fedha alizopewa na Matiko ili zikabidhiwe kwenye ofisi ya Takukuru Mkoa wa Manyara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles