25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

TOFAUTI YA UBORA WA JUISI, MATUNDA MWILINI

vegetable_juices_prevent_hair_fall

Na MWANDISHI WETU,

MATUNDA na juisi asilia, vyote kwa pamoja vina faida lukuki katika mwili wa binadamu, licha ya kwamba kimoja kinakuwa bora kuliko kingine. Hii inategemea zaidi mtumiaji anapenda nini au yuko katika hali gani kiafya.

hata hivyo kuna watu ambao kula matunda kwao ni mtihani, lakini juisi wanakunywa vizuri bila ya tatizo lolote.

Pia kuna baadhi ya watoto ambao wao kwa kawaida ni wavivu wa kutafuna, hivyo ili kuhakikisha kuwa wanapata virutubisho vilivyopo kwenye matunda, hakuna budi kuwatengenezea juisi.

Ikumbukwe kuwa matunda na mbogamboga ni ni miongoni mwa vyakula bora. Hii ni kutokana na wingi wa vitamini, madini, sukari ya asilia na virutubisho vingine.

Watu walio na matatizo ya kutafuna wanapokunywa juisi asilia hupata virutubisho hivyo kwa wingi zaidi katika glasi moja kuliko wale wanaokula kipande kimoja cha tunda.

Hivyo, juisi ni chakula kizuri kwa mgonjwa meno na Yule ambaye mahitaji ya nishati katika mwili wake ni makubwa.
Juisi hasa iliyotengenezwa na matunda halisi bila ya kuwekwa sukari au yenye sukari kidogo ina faida nyingi kwa watu wa rika lote – wazee, watoto na hata vijana.

Miongoni mwa faida za juisi ni kuongeza maji mwilini, kusafisha damu na kutoa sumu mwilini. Pamoja na mambo mengine, juisi ya matunda na mbogamboga husaidia mwili kuzalisha mkojo mwingi, hivyo kuondoa sumu mwilini pale mtumiaji atakapokwenda haja ndogo.

Juisi asilia pia ni kinywaji mbadala kinachoweza kumwepusha mtu kujenga mazoea ya kunywa soda au juisi za viwandani.
Wakati wa kutengeneza juisi, baadhi ya virutubisho muhimu wakati mwingine vinaharibika, vinapotea au vinaonekana kuwa ni uchafu na kutupwa.

Kuna baadhi ya matunda ambayo ngozi zake zinaweza kuliwa na ni chanzo muhimu cha virutubisho. Matunda hayo ni pamoja na tufaa (apple), blueberries, zabibu, strawberries, embe, pera na zambarau.

Ngozi ya matunda hupokea mwanga wa jua na kutengeneza virutubisho vyenye rangi mbalimbali ambavyo ni muhimu mno kwa ujenzi na ulinzi wa afya ya binadamu.

Mfano wa virutubisho hivyo ni carotenoids na flavonoids ambavyo vinasaidia kuimarisha kinga na afya ya mwili.  Vitamin C inahitaji uwapo wa flavonoids ili kufanya kazi vizuri mwilini.

Ngozi ya matunda kama zabibu zinasaidia kulinda afya ya ngozi ya binadamu na kupunguza hatari ya mtu kupata ugonjwa wa saratani.

Ngozi na nyama za ndani za matunda kama machungwa ni chanzo kizuri cha nyuzi lishe, ambazo hupotea wakati wa kuchuja juisi.

Nyuzi lishe zinasaidia usagaji wa chakula tumboni, humwezesha mtu kupata haja kubwa na kuepuka saratani ya utumbo mpana. Pia zinapunguza kasi ya sukari kutoka katika utumbo na kuingia katika damu, wakati huo huo zinapunguza wingi wa nishati.
Kwa hiyo, nyuzi lishe zinachangia kupunguza hatari ya mtu kupata ugonjwa wa kisukari, unene na uzito kupita kiasi.

Ulaji wa matunda na mbogamboga unajaza tumbo na kumfanya mtu kujisikia ameshiba kwa muda mrefu.  Juisi inaleta shibe ya muda mfupi na kuongeza nishati mwilini kwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles