23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

MAZOEA 10 MABAYA YANAYOWEZA KUHARIBU UBONGO

Ubongo
Ubongo

Na JOACHIM MABULA,

UBONGO ndio ikulu yako, huratibu na kusimamia kazi zote za mwili ikiwa ni pamoja na kuongea, kufikiri na kuvumbua vitu vipya. Watu wengi wanafanikiwa kiuchumi kwa kutumia vizuri ubongo wao ili uwaletee maendeleo. Kwa kutambua umuhimu wa ubongo katika maisha yetu, hatuna budi kutambua mazoea kumi yanayoharibu ubongo wetu bila ya sisi kujua.

 Kukosa mlo wa asubuhi

Watu wasiopata kifungua kinywa chenye lishe aina ya wanga na protini wanaweza kupatwa na upungufu wa sukari kwenye damu. Hali hii inasababisha ubongo kutopata virutubisho vya kutosha na kufanya ubongo kuanza kuharibika. Aidha, kukosa mlo wa asubuhi kunasababisha matatizo mengi ya kiafya ikiwamo kupanda kwa shinikizo la damu, kunenepa kupita kiasi na mpangilio mbovu wa mafuta katika damu.

Kukosa mlo wa asubuhi kunaufanya mwili ukae katika hali ya mkazo kwa kukaa njaa muda mrefu kwa sababu inapokuwa asubuhi unakuwa na shughuli nyingi na mwili unahitaji nguvu za kutosha, hivyo kukosa kifungua kinywa kizito kunaharibu utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kusababisha hali za hatari kwa afya ya mtu.

 Kula kupita kiasi

Mwili hutumia kalori zinazopatikana katika vyakula, kwa ajili ya utendaji wa misuli, ogani, tishu na seli. Kila mtu anahitaji kiwango chake cha kalori kwa kutegemea umri, jinsia, kimo, uzito wake wa sasa na aina ya kazi anayofanya. Kula kupita kiasi kunasababisha ateri za ubongo (mishipa ya damu iliyosheheni hewa ya oksijeni ambayo hutoa damu kwenye moyo na kuisafirisha kwenye ubongo) kuwa migumu hadi kupelekea kupungua nguvu ya akili. Aidha, kalori za ziada huhifadhiwa kama mafuta kwa matumizi ya baadae ingawa watu wengi hawatumii kalori hizo za ziada na kusababisha unene na kuzidi uzito.

 Uvutaji tumbaku

Uvutaji husababisha kusinyaa kwa ubongo kitu kinachoweza sababisha ugonjwa wa Alzheimer/Alzeima pia hujulikana kama udhaifu wa kiakili utokanao na uzee wa aina ya Alzeima. Ugonjwa huu usiotibika husababisha kupoteza kumbukumbu haraka zaidi. Wanasayansi wanadai kuna zaidi ya mchanganyiko wa kemikali 4,000 katika sigara. Kemikali za aina nyingi zina athari mbaya katika seli zetu, baadhi zinasababisha saratani na kufa kwa seli, hivyo uvutaji sigara unaweza kuua seli za ubongo pia.

Matumizi ya sukari kwa wingi
Ulaji wa sukari kwa wingi mfano vyakula vyenye sukari kama soda na juisi za viwandani unaingilia ufyonzaji wa protini na virutubisho vingine hivyo kusababisha utapiamlo unaoweza haribu ukuaji wa ubongo. Ulaji wa sukari kwa wingi katika mlo wako hakuta kuongezea tu uzito, bali utasababisha athari hasi kwenye afya ya mwili wako.

Mfumo wa ulinzi wa mwili wako ndio njia muhimu ya kuulinda mwili wa binadamu. Kutumia sukari kwa wingi kuna athiri utendaji wa mfumo huu na kupunguza uwezo wa kupambana na virusi, bakteria na vimelea vingine ambavyo vinaweza kuathiri ubongo pia.

 Kuufanyisha ubongo kazi wakati unaumwa

Ubongo ni moja ya ogani tata ya mwanadamu ikiwa na uwezo mdogo wa kujifanyiza. Ubongo ni rahisi kuathiriwa na ugonjwa. Kupoteza au kuharibika kwa mtandao wa seli za ubongo kunaweza sababisha athari kubwa hasa ukiulazimisha kufanya kazi wakati unaumwa. Kufanya kazi au kusoma sana huku unaumwa kunaweza kupunguza ufanisi wa ubongo pamoja na kuuharibu.

 Uchafuzi wa hewa

Ubongo ndio kiungo kikubwa kinachotumia hewa ya oksijeni katika mwili wako. Kuvuta hewa chafu kunapunguza usambazaji wa oksijeni katika ubongo na kusababisha kupungua kwa ufanisi wa ubongo. Kukaa sehemu yenye hewa nzuri kama mlimani au ufukwe mzuri kunaweza kuupumzisha na kuuimarisha.

 Kutosinzia vya kutosha

Kusinzia kunaruhusu ubongo kupumzika. Kujinyima usingizi wa kutosha kwa muda mrefu kutaongeza kasi ya kufa kwa seli za ubongo. Watoto wachanga wa chini ya umri wa mwaka mmoja wanapaswa kulala kwa kati ya saa 16 na 18 kwa siku, wakati wenye umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi mitatu wanahitaji saa 14.

Watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi minne wanahitaji kulala walau kati ya saa 11 na 12, wakati wenye umri wa kwenda shule, kwa maana ya miaka sita na saba, wanahitaji walau usingizi wa saa 10 kila siku, huku vijana wenye umri wa balehe na watu wazima wanashauriwa wapate usingizi wa kati ya saa saba na nane.

 Kufunika kichwa wakati umelala

Kulala huku umefunika kichwa mfano kwa wanawake wanaovaa kofia maalumu ili zisiharibu nywele walizosuka au kutengeneza kunaongeza msongamano wa hewa chafu ya kabonidioxide (dioksidi ya kaboni) na kupunguza oksijeni kitu kinachoathiri ubongo.

 Kukosa fikra chanya

Kuwa na fikra pevu ndio njia bora ya kuufunza ubongo wako, kukosa fikra chanya kunaweza kufanya ubongo kudhorota.

 Kuzungumza kwa nadra

Mazungumzo yenye busara yatachochea ufanisi wa ubongo wako. Ni vyema kutoa dukuduku lako kwa kuzungumza kila mara unapohisi kuwa unalo kwa sababu linaweza kuathiri afya yako kiujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles