25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

TNGP YALIA NA MAGUMU YA WANAWAKE

CHRISTINA GAULUHANGA NA ANASTAZIA MAGUHA (TUDARCO)-

DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa Mtandao wa Jinsia (TGNP), Lilian Liundi, amesema bado wanawake wanakabiliwa na changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia, huku akitaja Mkoa wa Manyara kuwa ni kinara wa vitendo hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Lilian alisema nguvu kubwa bado inahitajika ili wanawake waweze kujitambua na jamii iachane na mila potofu zinazochangia kuendelea kwa vitendo hivyo.

Alisema katika takwimu mbalimbali zinaonesha mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ni Manyara, Singida na Dodoma, ambapo elimu inahitajika kuiokoa jamii hiyo.

Lilian alisema katika kongamano  litakalofanyika Septemba 5 hadi 8 mwaka huu, watajikita katika kundi la wanawake ambao ni asilimia 51 katika jamii na vijana ambao ni zaidi ya asilimia 60 ili waweze kupata elimu na hamu ya kujikwamua kiuchumi.

“Katika kongamano hili tumepanga kuleta wanawake wengi ambao ni maarufu ili wanawake na vijana waone bado wana nafasi ya kujikwamua na kufanya mambo makubwa ndani ya jamii,” alisema Lilian.

Alisema pia watatoa elimu jinsi ya kufanya uamuzi, uwekezaji na ujenzi wa nguvu za pamoja ili wanawake waweze kujikomboa kiuchumi.

Lilian alisema tamasha hilo lililoandaliwa na TGNP na mashirika mengine binafsi, litahudhuriwa na watu zaidi ya 1,000 kutoka mikoa mbalimbali wakiwamo viongozi wa kiserikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles