Na Esther Mnyika Mtanzania Digital
MKURUGENZI wa Dawa za Binadamu na Mifugo kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Dk. Yonah Mwalwisi amezitaka kampuni zinazoagiza dawa kutoka nje na kuziingiza nchini kufuata taratibu zilizowekwa ili kumlinda mgonjwa.
Akizungumza leo Mei 12, kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wanaoingiza dawa nchini, Dk. Mwalwisi amesema uwepo wa mkutano huo ni kupata maoni yatakayoboresha mifumo yote ya uingizaji dawa nchini na uuzaji dawa nje ya nchi.
“TMDA kutoa ushauri kwa wadau walipokosea kwenye utendaji kunatararibu na sheria mbalimbali ambazo mfanyabiashara anatakiwa kuzifuata ikiwemo kupeleka cheti cha uchunguzi sambamba na dawa inapoingizwa nchini iwe imekaguliwa au kutoka kwenye nchi zinazotambulika na mamlaka hiyo,”amesema Dk Mwalwisi.
Amesema ili kuepuka ucheleweshwaji wa vibali vya huduma hiyo ambapo wamepokea zaidi ya maombi elfu 15 ya kuuza dawa na kusambaza
Amesema lengo letu kubwa ni kuendelea kumlinda mgonjwa ambae ndio mtumiaji wa bidhaa hiyo hawa wezetu wao wanaangalia namna ya ufanyaji wa biashara yao kwa ufanisi lakini sasa lazima tuwaangalie watumiaji wa mwisho wa bidhaa hiyo ambae ni mgonjwa.
Nae, Mfamasia wa kampuni ya Laborex Tanzania Limited, Geodfrey Yambayamba amesema mamlaka imeweza kuboresha mifumo mbalimbali ya usajili wa dawa na upatikanaji ambapo imewarahisishia kufanya biashara kwa urahisi.
“Kweli ni Kili sisi kama waagizaji mamlaka imetusaidia sana maana imerahisishia mfumo wa uingizaji wa dawa nchini kwa njia rahisi kwani sasa tunatuma maombi nje kwa kutumia mfumo na inatufanya tutumize malengo yetu ya kuhakikisha dawa zinapatikana kwa urahisi na haraka katika hospital zetu nchini,” amesema Yambayamba.