32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

TLS YAONJA SHUBIRI AICC, SASA KUHAMIA MT. MERU

Chama cha mawakili wa Tanganyika (TLS), kimelazimika kubadilisha ukumbi wa kufanyia mkutano wao wa nusu mwaka kwa mwaka huu, baada ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC), kuchukuliwa na mteja mwingine wiki mbili kabla ya mkutano huko.

Katika barua yake aliyoiandikia TLS, Mkurugenzi wa AICC, Elishilia Kaaya ameeleza siku hiyo ya Septemba 23, kuna mteja ambaye amechukua kumbi zote ukiwamo wa Simba ambao TLS walitarajia kufanyia mkutano wao ambapo pia amewaelekeza kama inawezekana kuahirisha mkutano huo hadi Septemba 30, ambapo ukumbi huo utakuwa wazi.

Hata hivyo, sekretarieti ya chama hicho imekiri kupokea barua ya kuwajulisha uamuzi huo ambapo imekubaliana na hatua hiyo na kuhamishia mkutano huo katika Hoteli ya Mt. Meru siku hiyo hiyo ya Septemba 23.

Aidha, sekretarieti hiyo ya TLS imewaelekeza wanachama mabadiliko ya mahali pa mkutano huo na kuelezea kuwa wasingeweza kubadili tarehe ya mkutano huo kwa sababu hiyo kwani wanachama wengi walishafanya maandalizi ya usafiri wa ndege na malazi mjini Arusha.

Baadhi ya wanasheria waliozungumza na Mtanzania Digital ambao hawakupenda majina yao yatajwe, wamesema hatua hiyo ni ya kisiasa lakini wao wanaamini katika kufanya kazi kitaaluma na kwa weledi.

“Tumekuwa tukitumia AICC miaka yote na ratiba yetu inafahamika vema, lakini kama sekretarieti ilivyoamua kubadilisha ukumbi ni kwa sababu tu ya maandalizi yaliyokwishafanywa na wanachama lakini kiuhalisia ukumbi wa Mt. Meru haukidhi kuchukua wanachama wote kwa wakati mmoja,” amesema mmoja wa wanasheria hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles