25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MWANAFUNZI ALIYENUSURIKA AJALI LUCKY VINCENT KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI

Mwanafunzi mmoja Wilson Tarimo, aliyenusurika katika ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32 wa Shule ya Msingi Lucky Vincent anatarajiwa kuwa miongoni mwa mashahidi 15 wa upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili mmiliki wa shule hiyo, Innocent Moshi.

Mmiliki huyo anakabiliwa na makosa ya usalama barabarani ikiwamo kusafirisha wanafunzi bila kuwa na vibali muhimu ambapo katika kesi hiyo namba 78 ya mwaka huu, Moshi ameshtakiwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Nkana ambao leo Septemba 11, wamesomewa hoja za awali katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru mkoani hapa.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Desderi Kamugisha, Wakili wa Jamhuri Khalili Nuda, amedai kuwa Jamhuri wanatarajia kuwa na mashahidi 15 katika kesi hiyo pamoja na vielelezo 12 ambapo amewataja mashahidi wengine kuwa ni Ofisa Kazi Mfawidhi wa Idara ya Kazi Mkoa wa Arusha, Wilfred Mdemi, Mohamed Matumula kutoka Kampuni ya Bima ya Zanzibar Insurance, Songoyi Jilala (Askari wa usalama barabarani Arusha), Koplo Hamad (Karatu), Inspekta Shukrani na Koplo Saada ambao ni askari wa usalama barabarani, mjini Arusha.

Wakili Nuda alitaja vielelezo hivyo kuwa ni kadi ya gari lenye namba za usajili T 871 BYS, mkataba wa ununuzi wa gari, Barua ya RTO kwenda Sumatra ya Mei 8, mwaka huu barua ya RTO kwenda Zanzibar Insurance ya Mei 8 mwaka huu, taarifa ya Zanzibar Insurance ya Mei 9 mwaka huu.

Akiwasomea hoja hizo za awali, Wakili Nuda amedai mahakamani hapo kuwa katika kosa la kwanza linalomkabili Moshi, ni kufanya biashara ya usafirishaji abiria bila kuwa na leseni ambapo kati ya Desemba 12 mwaka jana hadi Mei 6 mwaka huu, alitumia gari katika barabara ya umma  aina ya Mitsubishi Rossa T 871 BYS, kubeba wanafunzi, kosa la pili ni kuruhusu gari hilo kutumika bila kuwa na bima kati ya kipindi cha Desemba 16 mwaka jana na Mei 6 mwaka huu.

Kosa la tatu ni kushindwa kuingia mkataba na mwajiriwa wake kati ya Juni Mosi mwaka jana hadi Mei 6, Mwaka huu akiwa mmiliki  wa gari hilo alishindwa kuingia mkataba wa ajira kinyume na sheria za ajira na dereva wako Dismas Gasper ambaye kwa sasa ni marehemu. Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Septemba 28, mwaka huu.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles