28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Tino Mponzi: Mtanzania anayeutangaza mchezo wa karata za Albastini nchini Marekani

KARIBU msomaji wa safu hii ya inayokupa nafasi ya kufahamu mambo kadha wa kadha kutoka kwa watu maarufu na wadau wenye mchango chanya kwenye tasnia ya burudani.

Leo tupo na Tino Mponzi, Mtanzania anayeishi Marekani huku akijikita zaidi katika kuutanganza mchezo wa karata za Albastini kwenye nchi Ughaibuni.

SWALI: Karata ina michezo mingi, wazo la kufanya karata Albastini kwenye nchi za Ughaibuni ulilitoa wapi?

Tino Mponzi: Kusema ukweli Albastini nilifundishwa nilipokuwa mdogo na wazazi wangu wakati tupo Ethiopia na sikuwahi kukulia Tanzania hivyo mchezo wa Albastini ulitufundisha mambo mengi kuhusu Tanzania kama kuongea Kiswahili pia kwa sababu tulikuwa tunacheza na wazazi wetu.

Nilipokuja Marekani nilianza kuwaonyesha rafiki zangu jinsi ya kucheza Albastini, watu walifurahi sana kwahiyo nikaona bora tuirushe ili watu wengine nao wapate nafasi ya kuijua kwa sababu ni mchezo bora wa Kitanzania.

SWALI: Jambo gani lilikufanya uanzishe na kulitekeleza wazo hilo?

Tino Mponzi: Hiyo idea ilikuja baada ya mimi na wadogo zangu tulikuwa tukikutana tunacheza mpaka usiku sana kwahiyo tulisema ngoja tutengeneze njia ili tuweze kucheza tukiwa hatupo pamoja kwakuwa wao wanaishi mbali na mimi.

SWALI: Kwa mtu ambaye hakufahamu kama Mwasisi wa mchezo huu katika kuutangaza ughaibuni, wewe ni nani?

Tino Mponzi: Mimi naitwa Augustino Mponzi, naishi Dallas, Texas hapa Marekani, mimi ni Mtanzania lakini nimekulia nje kwahiyo sijawahi kuishi Tanzania.

Mimi ni mtoto wa kwanza kati ya watatu kwenye familia yetu, nina wadogo zangu wawili mmoja anaitwa Inock na mwingine ni Joseph, sisi tunatokea Iringa, wazazi wetu wote wawili wanatoka huko, shule ya msingi nilisoma Ethiopia, sekondari nilisoma Kenya na baada ya kumaliza masomo ya sekondari ndio nikaja Marekani kusoma Chuo Kikuu.

SWALI: Wewe ni mtaalamu wa IT, je elimu hiyo ndio ilikusukuma utumie teknolojia kuanzisha mchezo wa Albastini kwa njia ya mtandao na changamoto ilikuwa ni nini?

Tino Mponzi: Ndio ni kweli. Changamoto zilitokana na kutafuta namna ya kutengeneza kwa sababu hakukuwa na mtu mwingine ambaye nilikuwa namfahamu anayetengeneza mchezo wa karata, ilibidi nihakikishe kwamba wakati natengeneza nijifunze, ilichukua muda wa mwaka mmoja kutoa toleo la kwanza, mimi na wadogo zangu tuliweza kucheza.

Nikafikiria kama watu wengine wanataka kujiunga kwenye mchezo wetu wanafanyaje, ikabidi nifanye marekebisho zaidi kwahiyo baada ya hapo, nikafanya tafiti na nikatoa toleo la pili ambalo sasa watu wa mataifa mbalimbali wanaweza kujiunga kucheza.

SWALI: Umeuleta mchezo wa Albastini kwa njia ya App, umelenga watu wa aina gani wacheze?

Tino Mponzi: Tuna uhakika kwamba watu wengi wataingia, tulikuwa na wachezaji karibia 5,000 tulipotoa toleo la pili kwahiyo tunategemea kupata wachezaji zaidi tukitoa toleo la tatu itakayotupa nafasi ya kupata wachezaji zaidi.

SWALI: Mpaka sasa mmefanya mashindano mangapi ya Albastini?

Tino Mponzi: Tumefanya mashindano mengi, kama manne hivi na hatukufanya matangazo, tulirusha tu kuangalia nani anaikumbuka, watu wengi waliojiunga ni kutoka Tanzania, Ulaya na Marekani, tulikuwa tunatoa zawadi na tukashuhudia wataalamu kweli kweli wa kuicheza Albastini.

SWALI: Hapo Marekani Kuna michezo maarufu ya karata kama ile inayocheza kwenye kasino kama vile Uno na mingine, je wameupokea vipi michezo mpya wa Albastini?

Tino Mponzi: Wamarekani wameupokea vizuri sana, kuna mchezo unafanana na Albastini unaitwa state na Uno kama ulivyosema na ukilinganisha na Albastini kuna utofauti mkubwa sana na Wamerekani wamegundua Albastini inaongoza kwa ubora kuliko michezo mingine, tumefurahi sana tumenyanyua Tanzania na watu wajue kuwa tuna michezo mizuri sana.

SWALI: Unadhani mchezo wa Albastini unaweza kutumika kama kivutio cha utalii wa ndani Tanzania?

Tino Mponzi: Ndio unaweza kuwa kivutio cha utalii.

SWALI: Tumezoea karata za Albastini Zina karata 36 ila kwenye hii mpya kuna karata 72, kwanini?

Tino Mponzi: Tuliamua kufanya hivyo kwasababu karata 36 unaweza kucheza watu wanne hadi sita kiasi kwamba watu wanazingua karata mapema na ni rahisi kushinda kwahiyo tuliamua kuongeza karata hadi 72 sababu unawapa watu challenge kubwa zaidi na si rahisi sana kushinda pia unaweza kucheza na watu mpaka nane hiyo imeongeza ubora wa mchezo wenyewe.

SWALI: Uliweza vipi kuingia Kickstarter?

Tino Mponzi: Hilo ni jukwaa ambalo linaruhusu watu waingie kama wana idea, wakaweka project, sisi tiliingia Kicksty ili kutoa taarifa kwamba mchezo wa Albastini upo na tumeongeza namba za karata kutoka 36 hadi 72 na tuweze kuziweka mtandaoni.

SWALI: Tunamaliza mwaka na umesema kuna shindano ambalo litahusisha zawadi kwa Watanzania, imekaaje hii?

Tino Mponzi: Tuliamua kuzitoa karata hapa Marekani na Ulaya kwa sababu hizo ni sehemu ambazo hawazifahamu kabisa na Tanzania tumeitoa ile App na tuwe na shindano ambalo wataalamu wa kucheza Albastini na litafanyika kipindi cha Pasaka na App yenyewe itakuwa imetoka kabla ya shindano.

SWALI: Wapenzi wa karata Bongo watarajie nini zaidi kutoka kwako?

Tino Mponzi: Kwasasa natafuta fursa ya kuuza Albastini hii hapo Tanzania hiyo nadhani itakuwa 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles