29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi, Meneja Kampuni ya madini wanaswa kwa kuteka na kuomba rushwa mil 30

Na Mwandishi wetu,Arusha

Askari polisi watatu na raia sita akiwepo mfanyabiashara wa  madini, Lucas Mdeme, wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha, kwa tuhuma za kumteka na kumuomba rushwa  Mwenyekiti wa Chama cha wauzaji wa madini Tanzania(TAMIDA), Sammy Mollel .

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni, amesema tukio hilo limetokea Desemba 14, mwaka huu na kuwataja waliokamatwa kuwa ni Askari namba H.125 Gasper Paul  kitengo cha Intelijensia Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Meneja Kampuni ya Crown Lapidary, Lucas Mdeme moja watuhumiwa

Wengine ni Askari namba G 5134 DC Heavenlight Mushi wa kitengo cha Intelijensia Mkoa wa Kinondoni na Askari namba  H.1021PC Bryton Murumbe kutoka Dodoma.
Kamanda Hamduni aliwataja wengine waliokamatwa ni pamoja na Mfanyabiashara wa madini, Lucas Michael Mdeme(46) ambaye ni Meneja wa kampuni ya  kuuza madini ya CROWN Lapidary Ltd ya jijini Arusha, Shabani Benson(49) Mfanyabiashara wa Dodoma na Nelson Lyimo(58) Mfanyabiashara wa Kimandolu Arusha.

Watuhumiwa wengine ni Leonia Joseph(40) Sekretari wa kampuni ya Germs & Rocks Ventures, Omary Mario(43)mfanyabiashara wa eneo la Olorieni Arusha na Joseph Chacha(43) mfanyabiashara wa Elboru Arusha.

Amesema awali polisi iliwakamata watuhumiwa watatu, wakiwemo polisi wawili DC Muchi, PC Murumbe na mfanyabiashara Benson wa ofisi ya Germs & Rocks baada ya kuenda kushawishi na kupokea rushwa na baadaye kukamatwa watuhumiwa wengine sita.

Amesema taarifa za awali zinadai kuwa watuhumiwa hao, waliomba rushwa ya Sh milioni 30 na walipokea tayari fedha Sh milioni 10 na kiasi kilichobaki walipofuata ndio walikamatwa.                     
Mollel alikiri kukamatwa na watuhumiwa hao, ambao walikuwa na silaha na kuondoka nae kuelekea Dodoma na wakiwa njiani kabla ya kufika Dodoma ndipo waliomba fedha .

Hata hivyo, alisema kwa sasa hawezi kufafanua zaidi tukio hilo, kwani bado uchunguzi unaendelea na watuhumiwa bado wanakamatwa.

“Huu ni mtandao mkubwa wametapeli wafanyabiashara kadhaa hivyo vyombo vya usalama vinafayakazi,”alisema.

Mmoja wa watuhumiwa hao, Mdeme ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa TAMIDA na Meneja wa kampuni anayofanyakazi ya Crown Lapidary Ltd iliwahi kutajwa katika kesi ya Utoroshaji madini katika uwanja wa kimatataifa wa kilimanjaro(KIA).

Mfanyabiashara mwenye asili ya Asia, Raia wa India, Anarag Jain(44) akitorosha madini gramu 2015.59 yenye thamani ya dola 310,137.255 (Sawa na Sh milioni 670.

Baada ya kukamatwa  na madini kutaifishwa mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama ya mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga  aliitaja kampuni ya Crown Lapidey inayomilikiwa na raia wa Kenya, Rajan Verma kuwa ndio ambao walihusika kumuuzia mfanyabiashara huyo madini na kuahidi kumsadia kutorosha.

Mdeme alitajwa mahakamani kuhusika kuwarubuni maafisa wa usalama wa uwanja huo na wafanyakazi, Askari E.3985D/CPL Endrew, Caphace Rangia, Rachel Shao, na Debora Komba kumuingiza ndani ya uwanja huo lakini baadaye madini yalikamatwa.

Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles