26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Timu 64 kuchuana Bonnah Segerea Cup

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
 
TIMU 64 za soka kutoka mitaa mbalimbali ya Jimbo la Segerea zinatarajiwa kuchuana kuwania kombe katika mashindano yaliyoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo, Bonnah Kamoli.

Mashindano hayo yatakayozinduliwa Desemba 3 mwaka huu yanatarajiwa kuhitimishwa Januari 18 mwakani na yatachezwa katika viwanja vinane tofauti.

Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli, akikabidhi jezi kwa mwakilishi wa timu ya mchezo wa rede kutoka Kata ya Kinyerezi, Hadija Hamza (kushoto), wakati wa mkutano kuhusu mashindano aliyoyaandaa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Bonnah amesema mashindano hayo yanalenga kuibua na kukuza vipaji vya vijana sambamba na kuwapatia fursa mbalimbali.

“Nimekuwa nikiandaa mashindanio haya mara kwa mara, sote tunafahamu michezo ni afya, michezo ni ajira lakini pia kupitia michezo tutaweza kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yetu,” amesema Bonnah.

Amesema pia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo kutakuwa na mchezo wa rede utakaoshirikisha timu 13 ambapo kila kata itatoa timu moja.

Kwa mujibu wa Bonnah mshindi wa kwanza wa mashindano ya soka atazawadiwa Sh milioni 5 wakati mshindi wa pili atapata Sh milioni 3 na mshindi wa tatu atapata Sh milioni 2.
 
Naye Katibu wa Mbunge huyo, Rutta Rucharaba, amezitaka timu zote kudumisha nidhamu na kuonya kuwa ikithibitisha mchezaji anaishi nje ya Segerea au anashiriki ligi kuu ataondolewa kwenye mashindano hayo.

Mbunge huyo pia amekabidhi jezi kwa timu 13 zitakazoshiriki mpira wa rede na kwamba timu za soka zitakabidhiwa jezi wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles