27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yafuta matokeo ya uchaguzi wa UVCCM Simiyu, rushwa yatajwa

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefuta matokeo ya uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Simiyu kwa kilichodaiwa ni kuwepo kwa dalili wazi za rushwa.

Pia kimesimamisha uchaguzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kwa mikoa ya Arusha na Mbeya ambao wanaotuhumiwa kutembeza rushwa huku wakionya uamuzi wa kufuta unaweza kuendelea katika maeneo yatakayobainika kukiuka sheria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo, Jumatatu Novemba 21,2022 Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema leo ni siku ya tatu timu maalumu ya uchunguzi ipo huko ikichunguza zaidi kuhusu kilichojili ili vikao vifanye maamuzi.

Chongolo ametaja sababu kuu ni vitendo vya rushwa ambavyo vimetajwa katika maeneo hayo na kuwa chama hakitavulimia vitendo hivyo pale inapobainika.

Pia amesema wanachunguza kuhusu uchaguzi wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi.

“Katika tuhuma za kada mmoja kubeba boksi la kura kwenda nalo chumba cha kuhesabia kura ikibainika tutatoa maelekezo ama ya kufuta matokeo au kuruhusu aliyetangazwa aendelee,” amesema Katibu huyo.

Amesema hawako tayari kuona viongozi wanaingia madarakani kwa rushwa na vitendo viovu.

Amesema adhabu zitakazotolewa ni kuondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi na kupelekwa katika vyombo husika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles