Na Asha Bani, Mtanzania Digital
MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania(THRDC) Kanda ya Pwani ya Kusini kwa kushirikiana na Shirika la Door of Hope inaendesha warsha ya siku mbili ya kuwaongezea uwezo maafisa wa polisi na waendesha mashitaka kutoka kanda ya Pwani ya Kusini inayohusisha mikoa ya Mtwara,Lindi na Ruvuma.
Mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea uwezo maafisa wa polisi na waendesha mashtaka juu ya namna ya kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia,unyanyasaji wa watoto na masuala ya haki za binadamu.
Miongoni mwa matokeo yanayotarajiwa katika mafunzo hayo ni pamoja na mpango kazi wa pamoja utakaoandaliwa kuhusu njia zitakazotumika katika kushughulikia masuala ya haki za binadamu.
Pamoja na hayo washiriki watajadili namna bora ya kuongeza mashirikiano baina ya Polisi, Waendesha Mashtaka na Mashirika ya Haki za Binadamu.