28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wengi wapinga TICTS kupewa mkataba mwingine

*Washauri Serikali itafute Mwekezaji mwenye uzoefu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Zaidi ya asilimia 65 ya Watanzania hawakubaliani na kuongezewa mkataba kwa kampuni ya ya Kimataifa ya kuhudumia Makontena katika bandari ya Dar es Salaam (TICTS) huku asilimia 15 pekee ndio wakitaka kampuni hiyo iongezewe mkataba.

Aidha, asilimia18 ya waliotoa maoni wamesema hawajui. Maoni hayo yanaendeshwa na kuratibiwa na Ukurasa Maoni ya Wananchi kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Kampuni ya TICTS kwasasa inaomba kuongezewa mkataba baada ya ule wa awali wa kufikia ukingoni.

Hata hivyo, kwa kipindi kirefu sasa kampuni ya TICTS imeendelea kunyooshewa kidole kwa kuhusishwa na utendaji wa kiwango cha chini wa Bandari ya Dar es Salaam, ukilinganisha na bandari kama Mombasa nchini Kenya.

Kampuni hiyo inaelezwa kuwa utendaji wake umekuwa sio wa kiwango cha kuridhisha nakwamba hakuna sababu za kuendelea kufanya kazi na kampuni ya namna hiyo kwa maslahi mapana ya Taifa.

“Imebebwa miaka mingi, matatizo ni hayohayo ufanisi chini ya kiwango itangazwe tenda wapewe wengine,” amesema Frank Peter.

Upande wake, Ayubu Kivaula amesema kuwa: “Kampuni hiyo nashauri iangaliwe upya kabla ya kuongezwa mkataba mpya,” amesema Frank Peter.

ACT Wazalendo

Chama cha ACT Wazalendo kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa, pia kimeitaka Serikali isitishe nyongeza ya mkataba huo kwa sababu mbalimbali ambazo kimeziainisha.

ACT inasema kuwa moja ya sababu kubwa ni malalamiko ya muda mrefu ya wafanyabiashara na waagizaji, ambao wamekuwa wakibeba mzigo wa gharama za uchelewaji wa kufunga meli na kuondosha mizigo.

“Mfano Chama wa Mawakala wa Forodha (TAFFA) wamekuwa wakilalamika miaka nenda rudi kuhusu TICTS kuwa na ufanisi mdogo na kusababisha ucheleweshaji wa mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam.

“Malalamiko haya yamethibitishwa na repoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) karibu kila mwaka. Mfano ripoti ya CAG ya mwaka 2020/21 inaonyesha kuwa kuna ucheleweshaji wa ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam jambo linasababisha malalamiko ya wateja na kuathiri ufanisi wa utendaji wa bandari.

“CAG alionyesha meli za mizigo na mafuta zinachukua wastani wa siku tatu hadi nane kupakua mizigo kinyume na mipango ya mamlaka ya bandari ya kuhakikisha inapunguza hadi kufikia siku mbili,” kinabainisha chama hicho na kuongeza kuwa:

“Ucheleweshaji huu na utendaji hafifu wa TICTS unasababisha meli kukaa muda mrefu bandarini na kunaathiri utendaji na ufanisi wa bandari kwa ujumla,” kinaeleza chama hicho.

Ikumbukwe kuwa Aprili mwaka huu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alinukuliwa na vyombo vya habari akitoa agizo kwa kampuni hiyo kuimarisha utendaji kazi wake ili kuondoa kero ya ucheleweshaji wa mizogo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Kama hiyo haitoshi, hivi karibuni, Rais Samia Suluhu Hassan aliikosoa hadharani Bandari ya Dar es Salaam kwa kukosa ufanisi na kumfukuza kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eric Hamissi, na kumteua, Plasduce Mbossa ambaye ameahidi kuongeza ufanisi wa bandari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles