23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia awakumbuka Mashujaa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amependekeza kwa ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, kutenga eneo kubwa na bora zaidi kwa ajili ya kujenga mnara wenye hadhi ya makao makuu.

Kauli hiyo ameitoa leo Julai 25, 2022, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa katika viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma, ambapo pia ameshauri kwamba maadhimisho ya namna hiyo yawe na gharama nafuu.

“Kwa kuwa Jiji la Dodoma linakua, nipendekeze kwa Waziri Mkuu, ofisi yako pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoma kutafuta eneo kubwa na bora zaidi ili kujenga mnara wenye hadhi ya makao makuu ya nchi kwa gharama nafuu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ametumia siku hiyo kuwakumbuka mashujaa hao na kusema kwamba mchango wao utaendelea kuenziwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles